QYT YAENDELEA KUPANUA HUDUMA ZAKE JIJINI DAR ES SALAAM



 Kampuni ya QYT inayojihusisha na huduma za tiba mbadala pamoja na kutoa fursa Kwa vijana, imeendelea kupanua miradi yake Kwa kufunga tawi jipya katika kata ya mwananyamala wilaya ya kinondoni Jijini Dar es salaam.

Ufunguzi wa kituo hicho umeambatana na semina za Afya Kwa wakazi wa eneo Hilo namna ya kujikinga na maradhi yasiyo ambukiza kama kisukari na pressure ambayo yamekua yakiongezeka Kwa Kasi kubwa nchini.

Mkurugenzi wa QYT Tanzania Bw. Laurence Steven amesema kampuni hiyo imelenga kutoa huduma Bora zaidi za kiafya na elimu Kwa umma kuhusu kutambua wajibu wa kujikinga na maradhi yasiyo ambukiza yanayoongezeka Kwa Kasi kubwa nchini hasa Kwa watu wazima.

Kwa upande wake Judith Mwaheleja Kwaniaba ya kituo hicho amewakaribisha wananchi wa wilaya ya kinondoni na maeneo mengine kupata huduma Mahali hapo ikiwemo vipimo vya mwili mzima (Body Checkup) Kwa gharama ya elfu ishirini pekee.

Huduma zingine ni pamoja na matibabu ya maradhi yasiyo ambukiza Kwa kutumia virutubisho vya asili na huduma zingine za kutoa sumu mwilini. Amesema Bi. Judith







About life goes on

Blogger | Journalist | Entrepreneur | Fashonista Based in Dar es Salaam, Tanzania.

0 comentários :

Post a Comment