DASH COMMUNICATION

DASH COMMUNICATION

ZANELLE BONGO LADIES WEAR

ZANELLE BONGO LADIES WEAR

ANDY BEACH

ANDY BEACH

AK

AK

NASAROG

NASAROG

NAKEMEA MAUAJI YA ALBINO

NAKEMEA MAUAJI YA ALBINO

Baby shop

Baby shop

COCO BEACH

COCO BEACH

RJ

RJ
Home » » HISTORIA YA MAISHA YA WEMA SEPETU

HISTORIA YA MAISHA YA WEMA SEPETU

 
Wema Sepetu alizaliwa tarehe 28, September, ni mtoto wa mwisho kati ya mabinti wanne wa Mzee Sepetu.
Wema hakufikiria kama atakuja kuwa mmoja kati ya ma-star wakubwa hapa nchini hadi nchi za nje mpaka siku mmoja alipo kuwa kwenye matembezi yake Slypway Masaki alikutana na dada Mange Kimambi na kushawishiwa ashiriki mashindano ya Miss Tanzania 2006...
 Wema Sepetu aliibuka kidedea na kuwagalagaza Jokate Kidoti Mwegelo na Lisa Jensen

Kabla ya kuwa miss Tanzania alikuwa na mwandani wake japo hakuwa super star lakini hawakudumu maana aliposhikilia taji alikuwa busy jambo lililomfanya akose muda wa kumpa mwandani wake lakini muda mchache akakutana na Marehemu Kanumba na kuanza uhusiano mara moja....
Uhusiano baina ya Kanumba na Wema ulikwenda vizuri sana nakama mchezo nyota zao zote zikang'aa sana Kanumba sasa akaonekana Kanumba kweli si yule wa kwenye maigizo ya kikundi cha Kaole tena uhuu ni ukweli kabisa.. na haswa waliposhirikiana katika movies zao walizidisha umaarufu mara dufu, lakini kiukweli ni kwamba Kanumba ndiye aliye gundua kipaji cha Wema na ndiyo aliye muibua katika sanaa ya kuigiza.
Wema sijui ni utundu au utoto au ulimbukeni wa mapenzi basi akamsaliti Marehemu Kanumba na kuwa na mvuta bangi Jumbe.
 
 Pichani ni Wema na mpenzi wake Steven Kanumba enzi za uhai wake Kanumba (RIP)

Kwakweli katika mapenzi yote nazani alipochemsha binti wa Sepetu ni pale alipokuwa na Jumbe maana ilimpelekea hadi kuwekwa rumande. Natusinge angalia Wema naye angekuwa mvutaji bangi na madawa ya kulevya


Wema mahakamani akiwa na mpenziwake wa zamani Jumbe

Wazazi wake haswa mama mtu alijitahidi sana kumuokoa Wema kwenye mikono mibaya ya Jumbe
 Heka heka za Wema wa Sepetu hazikuishia hapo akajikuta mikononi mwa Chalz Baba kaka yangu na mie huyooo

 Wazazi wakaona basi tena maana mwanao kutwa magazetini wakampeleka Ulayaaaa...sasa akiwa marekani kwa mmoja wa dadazake huko alikuwa anachati na watu kwa kutumia mitandao ya kijamii hii chating ya kwanza ya Wema na Diamond ilikuwa kwenye FACEBOOK siku hiyo mtoto wema alikuwa anacomment kwenye wall ya Diamond kimahaba huku mtoto wa mbagala akijibu mashambulizi asije poteza bahati
Mara Wema anasema mtu kifudenge naona kachoka a reply sasa hivi ....ikitajwa hivyo Diamond ana jibu akijijua yeye ndio mtukifudenge
Dah! enzi hizo diamond alikuwa kituko jamani hajulikani kabisaaaa watu mkisikia wimbo mkali wa mbagala mnatafuta aliyeimba nani mnakuta kituko mnabakia lakini anaimba vizuri.


Wema Sepetu alipotua tu inchini alifikia kupanga na kumkaribisha mpenzi wake mpya Diamond na kuanza maisha ya pamoja ya raha na mstarehe.....
Kwakweli watanzania wengi walipigwa na butwaa kila mmoja alilalama why Wema akachukua kinyarika kama hicho na mengi mabaya juu yao.
Nausifu sana ujasiri wa Wema kwani aliweka pamba masikioni na kutaka kutudhihirishia kuwa Naseeb aliyempenda yeye ni Almasi ...Diamond ambayo inang'aa duniani kote.
Hapa tunaona kabisa japo Diamond Platnum alishatoka na nyimbo zake kama mbili hivi kali moja wako ya Mbagala lakini hakuwa juu kiasi hicho na bila Wema angebakia kama wasanii wengine wanatesa na nyimbo kali ila nyota hazing'ai kivileee Ben Pol, Chid Benzi Barnaba na wengineo.
Wema hakuona haya kumpenda hadharani Diamond alimpiga mabusu hadharani watu wakapaka sana domo na mengineyo mengi lakini alizidisha mapenzi mara dufu. Ndipo tukaanza kumuona Diamond muonekano wa pili aling'aa sana akawa na swaga za Wema, kiingereza kidogo kila mwanamke akatamani awe kama Wema na Diamond wakawa hadithi tamu midomoni mwa watu navile mtoto Wema anavyojua kudeka na kupenda watu wakachanganyikiwa na mapenzi yao yalivyo noga.
Tutashangaa sana kwanini awali watu hawakupenda na wengine walimcheka sana Wema kuwa na Diamond lakini sasa jamii nzima inataka kusikia kwamba Wema amerudiana na Diamond...umeona eheee?
Mtu wa karibu na madam alininyetisha kwamba Wema alimpenda kwa dhati Diamond japo alipigwa vita sana na jamii kuwa hafai na si wa hadhi yake lakini hakuvunjika moyo alimpenda zaidi Diamond nakutufanya watanzania wote na ulimwengu wote kumtambua Diamond na kipaji chake na hadi tukamuona handsome wakati alikuwa hatazamaniki eti leo hii amekuwa super star anajidai kumbwaga na kumsaliti tena na kutembea na mashoga wa Wema kwakweli hii haijakaa sawa kabisa..hatuwezi kuwaacha walale na huyo kinyago wake Penny asiye kuwa hata na aibu namshangaa bado analazwa kwenye mashuka ya Wema na anakubali kwanini kama anampenda asimletee mengine wakalala ndio tuwaache..Diamond ni wa Wema tu labda arudie ule uchokoraa wake wa zamani wa mbagala ndio tutamucha sasa nao wamchukue wamng'aishe tuone kama watamgombea tena alisema kwa huzuni mnyetishaji.
     Wema Sepetu amezidi kupata umaarufu japo magazeti mengi yakiendelea kumchafua usiku na mchana lakini ni binti ambaye aseme leo atakuwa jangwani anayetaka kumuona aje basi hakika maelfu ya watu watakusanyika hapo nyota yake kwakweli iko juu mno ndio mana kila atakaye mshika mkono naye lazima awe juu na hii si kwa wanaume wake ni hata mashoga zake wa kike mfano halisi ni Snura.
  Pamoja na Wema kusemwa sana magazetini na kusalitiwa mara nyingi na kusemwa vibaya na mashoga zake na yote hayo lakini bado yuko juu kwani binti huyu ana kampuni yake ya production inayoitwa Endless fame na bado anakipindi chake ambacho hivi karibuni kinategemewa kurushwa hewani kitakachoitwa Reality Show na anajiweza imaisha na Mungu anazidi kumbariki kwani anajitoa sana kwa watu na sadaka, anamiliki nyumba na magari kwakweli Wema Sepetu you shine like diamond... your a star isiyo fifia.

Ombi kwa dada Wema ni kwamba achana na Diamond hakufai anataka kukumaliza tu ili akae pembeni akucheke anatambua kabisa ulimwengu mzima wote unajua ameng'ara kwa kupitia nyota ya Wema sasa anataka akuzime ili apate kutawala yeye achana naye bwana fanya ya maendeleo atakutafuta mwenyewe kwanza mnapo weka story kila siku Wema na Diamond ndio unamsaidia auze kazi zake maana akitoa nyimbo kila mmoja anataka ajue safari hii anamwimbia nini Wema yaani hauzi bila ya jina lako kama umemshtukia akiwa anatoa album au wimbo ndio zinakuja skendo za Wema na Diamond inamaana ndio muda huo huo anapo tafutia skendo auze yeye kwa kukupitia mgongo wako.

5 comments:

Anonymous said...

jamani kweli wema ni kama jina lake bwana watu atumtaki penseli coz penseli alikuwa rafiki wa uyu mtu jamani atumtaki msaliti

Anonymous said...

LILE LI PENNY LIKO KAMA GUMEGUME YAANI HALINA MVUTO BASI NA HUYO DOMO NI VITUKO TU WEMA SEPETU UKO JUU ACHANA NAO FANYA YAKO MAMA

Anonymous said...

wema wewe ndio nyota ya daimond kwa hivyo dada usibabaike na vidudu watu,love u wema

Anonymous said...

NI MATOKEO YA KUTUMIKISHWA NA MIKATAMBA YA KISHETANI KAMA VILE FREEMASON NA KWENDA KUZIMU KUCHUA KIBALI CHA KAZI - OLE WAO WANAO MSUJUDIA SHETANI WAPATE MALI NASEMA OLE WAO YUPO MUNGU KINYUME NA USHETANI WENU HUO.{Mbona mnadhalilisha uislam?? kama mtume mhamed ameshidwa kuwasaidia simjaribu kurudia Yesu Kristo????}KUNA HUKUMU YA JEHANA NA PIA KUNA UKIMWI

Anonymous said...

WEMA NAOMBA NAFASI MOYONI MWAKO NINAOMBA UNITAFUTE MUMY MR ABEL-0752238295- NITAKUPA ZAWADI YA KIPEKEE SANA

Post a Comment

 
Supported by : Jeedy Girl
Copyright © 2012. life goes on - All Rights Reserved
Modified by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Jeedy Girl