DASH COMMUNICATION

DASH COMMUNICATION

ZANELLE BONGO LADIES WEAR

ZANELLE BONGO LADIES WEAR

ANDY BEACH

ANDY BEACH

AK

AK

NASAROG

NASAROG

NAKEMEA MAUAJI YA ALBINO

NAKEMEA MAUAJI YA ALBINO

Baby shop

Baby shop

COCO BEACH

COCO BEACH

RJ

RJ
Home » » KANUMBA THE GREAT

KANUMBA THE GREAT

       Siamini hadi hii leo kama Kanumba ametutoka! pia siamini kwamba watanzania walikuwa wanampenda mno marehemu Stevin Charles Kanumba na kwamba wanazikubali kazi zake na wanauona mchango wake mkubwa katika jamii.
       Kwakweli nimesikitishwa na hilo badala ya kuwa na furaha nimeuzika kupitiliza hivi watanzania tutajikubali lini? Tutakuwa tunasubiri watu wafe ndio tuwaenzi na kuwasifu na kushangilia ushujaa wao au!!!!!

IMG_20120410_120103.jpg
UMATI WA WATU KATIKA KUMUAGA MAREHEMU KANUMBA 


JAMANI TULIKUWA WAPI SIKU ZOTE????????
       Watanzania wenzangu nafahamu fika hata siku moja hatukuweza kumpa sifa ndugu yetu mpendwa Kanumba zaidi ya kumbeza na kumpiga vita, na kaka wa watu alikazana kutuelimisha tufahamu mchango wake lakini tulikataa kata kata. Alijaribu kutuonyesha anaweza na anaitaji msaada kutoka kwetu natena si kifedha bali upendo na sapoti lakini bado tulimnyima.
        Nakumbuka mwaka juzi kama sikosei alipoweza kuingia ndani ya mjengo wa BBA nahisi alijuta kwenda huko. ohoooooo! zihaki matusi vicheko na kashifa vilitawala juu yake. Alijitahidi sana mumwelewe Watanzania wenzake kuwa anaweza apewe nafasi na mshirikiane penye mapungufu mumwelekeze badala ya kumbeza lakini hatukuweza kumsikiliza.
       Marehemu Kanumba alijua fika Watanzania hawampendi na hawataki kumkubali japo kazi zake ni nzuri kabisa alifahamu kabisa Watanzania wamejaza chuki juu yake ndio maana aliimba wimbo kuelezea kuwa siku atakapo kufa ndipo mtalia KANUMBA WETU UKO WAPI. (tafuta huo wimbo uusikilize kwa makini) pia kudhihirisha haya siku moja kabla ya kifo chake marehemu Kanumba aliwaelezea watanzania na dunia nzima kiujumla kupitia tovuti yake ya http://kanumbathegreat.blogspot.com/ kuwa WANYAMA JAPO HAWANA AKILI LAKINI WANAPENDA IWEJE SIYE BINADAMU WENYE AKILI TENA TIMAMU TUSIPENDANE?
 nazani ni moja ya maneno ya mwisho ya super star marehemu STEVE KANUMBA.
(Look at this pic careful,,,moja ya vitu tulivyotofautishwa na wanyama na ndege ni Akili ya kujua mema na mabaya,tizama hao ndege na huyo mbuzi hawana akili kabisa lakini wanapendana ndio maana unaona wako pamoja ILA binadamu aliyepewa akili ana roho mbaya sana,katika mafundisho ya YESU KRISTO alisema neno kuu nawapeni PENDANENI.hata uwe na uwezo wa kuhamisha milima kama huna upendo ni bure,mpende jirani yako kama unavojipenda,upendo haujivuni,hauhesabu mabaya,hautakabari,hauhusudu.....nk,1WAKORINTHO 13.Mungu ana akili sana kutuumba kwa mwili huu wa nyama laiti kama angetuumba kwa vioo au sightmirror ili uweze kuona mwenzako anakuwazia nini?anakufanyia nini?anapanga nini juu yako ungekuta ni heri ukaishi msituni na wanyama wakari kuliko kukaa na binadamu,katika tafiti zangu nimegundua kuna dawa mbalimbali mfano ya kichwa,homa,nk Lakini dawa ya Chuki na roho mbaya hakuna,,kama hiki kingekuwa kipindi kama kile cha zamani za Sodoma na Gomora au cha Nuhu ambacho Mungu alikuwa akiadhibu hapo hapo watu wengi sana wangeumbuka hasa wale wanaojifanya wasafi usoni lakini rohoni ni tofauti,Mungu atusaidie sana hasa sisi vijana tujue kusimama katika ukweli na uwazi,tuubebe upendo wa dhati toka rohoni huku mdomoni tukitamka amani ya kweli impendezayo Mungu ili watoto wetu waje watuenzi kwa mazuri na dunia ijivunie uwepo wetu.)


         Saa nyingine naweza kukubaliana kabisa na watu wanaosema kanumba alijua atakufa na ipo siku watu watajutia kumkosa. Namaneno hayo yalitimia dakika chache alipopoteza maisha.
watuwalilia na kusaga meno wakiomba arudi japo dakika moja wamsifie. wengine walidiriki kusema ni moja ya movie tu na kuwa kanumba hajafa kweli. Mamia ya watu walifurika wakiimba nyimbo zote za sifa na ushujaa wake na wengine kuzimia kabisaaa. 
    IMG_20120410_120301.jpg
MOJA YA WALIOZIMIA SIKU YA KUMUAGA KANUMBA
         
           Jamani! tulikuwa wapi wakati yuko pembeni yetu? mbona hata marafiki tulimgeuka na kumkana na kumbeza na kumsema na kumkataa na kumkimbia na kumtukana?
           Hili ni fundisho kubwa kwa watanzania. Nawaomba watanzania wenzangu tujifunze kupendana kupenda kazi za Tanzania Kuinuana Watanzania wenyewe kwa wenyewe. Tuache kabisa kuoneana wivu kuwa na mioyo ya chuki why huyu kapata???? tuache wapendwa. TUSIFIE KABLA HAJAFA.
           Nilivutiwa na jinsi watu wanavyomshangilia DIAMOND kwakweli iliniburudisha kuona sasa watu wamejifunza kutokana na makosa kwakweli nazidi kumuita marehemu KANUMBA ni shujaa maana pale pale kwenye msiba watu wakaanza kumshangilia Diamond inamaana walifunguka wakatoa haya zao wakamuonesha hata yeye wanamkubali.
           Nchi za wenzetu ukiwa super star ni super star kweli yaani mtu unapata moyo faraja yakuongeza juhudi katika kazi ilihali watu wazidi kukukubali. Unapata moyo kwa kweli.
TUJIREKEBISHE WATANZANIA.

                                       R.I.P KANUMBA
Kanumba The Great

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by : Jeedy Girl
Copyright © 2012. life goes on - All Rights Reserved
Modified by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Jeedy Girl