MATAASISI Na Mashirika dini ya Kiislam yametakiwa kuwapa vipaumbele Vijana Wa Kiislam katika Safari za Kuwadhamini katika safari ya ibada ya Ummra.
Akizungumza na Waumini wa Dini ya Kiislam Waziri Wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu( Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu Ridhiwani Kikwete Wakati wa Iftara Gala iliyoandaliwa na Taasisi ya "Sisters in Iman" Jijini Dar es Salaam amesema Jamii inapaswa Kuwapa Vipaumbele Vijana ili Kusaidia Vizazi vingine vijavyo katika kutafuta fursa mbalimbali hasa za Uongozi.
"Ili Kuimarisha Maadili lazima yaanzie na Vijana ambapo ndio msingi mzuri kwa Malezi mazuri Kwa vijana wa baadae hivyo Kupewa fursa kwa Vijana."
Hata hivyo amewapongeza Taasisi hiyo kwa kuona haja ya Vijana Kwenda Kuhiji inaleta taswira nzuri na kupunguza Mmomonyoko wa Maadili katika jamii. "
Hata hivyo Kikwete ameendesha zoezi la Kuchangisha fedha kwa lengo la Kusaidia Kundi lenye uhitaji wakiwemo watoto yatima,Wamama Wajane,Walemavu na Wazee.
Pia ametoa rai Kwa Wanawake wa Kiislam Kujitokeza kugombania Nafasi katika Nyazifa mbalimbali za Kiserikali ili kuendelea Kuimarisha maadili ya dini hiyo katika Jamii.
Kwa Upande wake Mwanzilishi wa Taasisi hiyo Dkt.Salma Iddy amesema Kwa mara ya Nne inafanyika Sherehe hizo za "Iftar gala" kwa lengo la Kuwatambua Wanawake wa Kiislam katika harakati zao na Shughuli zao Kidini.
Iddy ameongeza kuwa kwa Mwaka huu wametambulisha Gazeti lao ambalo limewatambua Wanawake mbalimbali katika Siasa,Biashara na nyanja nyingine ambao wamekuwa wakiwatia moyo Wanawake na Wasichana Wadogo Kuendelea Kujikwamua Kiuchumi na Kuishi ndoto zao wakiwa Kama Watu wanaowahusudu zaidi.
Nae Mwenyekiti Wa Taasisi hiyo Khadija Mjata ameongoza kuwa Taasisi hiyo ikishirikiana na Wadau Mbalimbali Wameamua Kuanzisha Mfumo mzuri utakaowawezesha Vijana Wadogo Kupata ufadhili wa Kutimiza Ibada za Hija na Ummra ambapo Taasisi ya Sister in Iman itagharamia hilo.
Pia ametoa wito kwa Wadau mbalimbali katika Mwezi huu Mtukufu Kusaidia watu wenye Uhitaji na Makundi mbalimbali.

0 comentários :
Post a Comment