Viongozi waliokutana na Mhandisi Andrew Kisaka uliongozwa na Katibu Mtendaji wa TBN Khadija Kalili ,Kaimu Mwenyekiti TBN Rwehabura Rugambwa ,Mweka Hazina Beda Msimbe na Wajumbe Muhidin Issa Michuzi, Frank Wandiba, Carren Mgonja na Shaaban Lulela .
Mamlaka ya wasiliano Tanzania (TCRA) leo tarehe 19.03.2025 imekutana na na Uongozi wa Tanzania Bloggers Netwark (TBN) katika Ofisi za TCRA Makao Makuu Jijini Dar Es Salaam.
Na Mwandishi Wetu
Katika kikao hicho TBN imeiomba TCRA kupunguza gharama za usajili wa Blogs kama siuo kuziondoa kabisa.
Aidha TBN imeiomba TCRA iwe inatoa mafunzo ya mara kwa mara kwa Bloggers ilikuwajengea uzoefu katika kazi zao za kila siku.
Baada ya kusikiliza maombi hayo Meneja wa Huduma za Utangazaji TCRA Mhandisi Andrew Kisaka amesema wameyapokea maombi ya TBN na watayafanyia kazi huku ameahidi kutoa mrejesho.
Mhandisi Kisaka ambaye ndiye alikua mwenyeji wa msafara huo wa Viongozi wa TBN amesema kuwa kwa niaba ya TCRA,
Mhandisi Andrew Kisaka akifafanua jambo mbele ya kamati ya Uongozi TBN iliyofika ofisini kwake leo tarehe 19.Machi.2025 Jijini Dar es Salaam."Tunafurahi kukutana nanyi leo na kujadiliana mambo mbalimbali sambamba na kutambua namna mnavyoendesha shughuli za kihabari maana Bloggers mna umuhimu mkubwa sana kwenye maudhui ya ndani na kwa mustakabali wa nchi kwa ujumla hivyo ninawaahidi kuwa tumepokea maombi yenu, tutayanyia kazi na majibu tutawapatia" amesema Mhandisi Kisaka.
About life goes on

Blogger | Journalist | Entrepreneur | Fashonista Based in Dar es Salaam, Tanzania.
0 comentários :
Post a Comment