

Katika hatua nyingine, alizungumzia kauli mbiu ya Mkutano huo, 'Wajibu wa Vyombo vya Utangazaji kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025', na kuwasihi waandishi wa habari kutumia taaluma zao kusimamia haki na usawa katika kuhabarisha umma, huku wakizingatia weledi, sheria, na kanuni za utangazaji.
Alisisitiza pia waandishi wa habari kuepuka habari za kugushi, hasa kwa kuzingatia mabadiliko ya kiteknolojia katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu, ili kuepuka kupotosha umma au kuleta taharuki.
Prof. Kabudi ametoa pongezi kwa waandishi wa habari kwa juhudi zao za kuhabarisha umma kuhusu taarifa mbalimbali za serikali, ikiwa ni pamoja na Mkutano Mkuu wa Nishati uliohudhuriwa na Marais kutoka nchi mbalimbali, uliofanyika jijini Dar es Salaam, na akawasihi waendelee kuelimisha wananchi kuhusu jinsi ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kwani hiyo ni ajenda ya kitaifa.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui, Saida Muki, amesisitiza kuwa waandishi wa habari wanapaswa kuwa makini na matumizi ya Teknolojia ya Akili Bandia (AI) wakati huu wa kuelekea Uchaguzi Mkuu ili wasiwasilishe maudhui yanayoweza kupotosha umma.
Msemaji Mkuu wa Serikali, Grayson Msigwa, amewashauri waandishi wa habari kuwa, kupitia Mkutano huu, wanapaswa kuzingatia weledi katika taaluma yao hasa kuelekea Uchaguzi Mkuu ili kulinda usalama wa taifa.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dkt. Jabir Bakari, amesema mkutano huu umeandaliwa ili kujadili masuala muhimu yanayohusu sekta ya habari na kutafuta ufumbuzi wa changamoto zinazokikabili sekta hiyo.
Akizungumzia Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu, Dkt. Bakari amewasihi waandishi wa habari kutumia taaluma zao vizuri, kuhabarisha umma kuhusu hatua zote za uchaguzi hadi siku ya kupiga kura.
Baadhi ya waandishi wa habari wameelezea kuridhishwa na hatua ambazo serikali imekuwa ikichukua katika kuimarisha sekta ya habari.


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na michezo mhe Palamagamba Aidan Mwaluko Kabudi amezungumza na kuweka msisitizo ambao amesema kuwa matumizi mabaya ya Utangazaji na utoaji wa habari ambazo zisizo na Ueledi zinavyoleta Athari kubwa katika Dunia na Kuleta mifarakano
About life goes on

0 comentários :
Post a Comment