Benki ya NBC Yachochea Ukuaji Sekta ya Michezo, Burudani na Utalii Zanzibar, Rais Samia, Dkt Mpango Wapongeza.


Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) mwishoni mwa wiki ilishiriki kikamilifu kwenye Tamasha la Kizimkazi Zanzibar kwa kuandaa matukio kadhaa ya kimichezo, burudani na utalii visiwani humo yaliyohusisha uwepo wa viongozi wakuu wa nchi wakiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango na viongozi wengine waandamizi wa serikali.

Katika matukio ya michezo benki hiyo kwa kushirikiana na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) walishikirikiana kuandaa tamasha kubwa la muziki lijulikanalo kama “Bongo and Zenji flavour night” lililofanyika Paje likihusisha uwepo wa Rais Samia. Tukio hilo lilitanguliwa na mechi ya fainali ya ligi ya soka ya Vijana wa Kizimkazi ijulikanayo kama “Samia Kizimkazi Youth Cup” iliyofanyika Uwanja wa New Amaan Complex iliyoongozwa na Makamu wa Rais, Dkt Mpango.

Fainali hiyo ilihitimishwa kwa timu ya Shule ya Sekondari Kusini kuibuka mabingwa wa kombe hilo baada ya kuifunga Shule ya Sekondari Muyuni jumla ya magoli 3-0. Katika kukabidhi zawadi kwa mabingwa hao vijana, ilishuhudiwa Makamu wa Rais, Dkt Mpango akiwaongoza wadau wengine wakiwemo viongozi waandamizi wa serikali pamoja na wadhamini wa ligi hiyo kampuni ya Mawasiliano TTCL na benki ya NBC walioongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Theobald Sabi

Akizungumzia kwa ujumla matukio hayo wakati wa uzinduzi wa mradi wa utalii wa Samaki aina ya Kasa uliopo kwenye Pango la Salaam (Salaam Cave) katika Shehia ya Kizimkazi Mkunguni uliodhamininiwa pia na benki ya NBC kwa ushirikiano na TTCL, Rais Samia pamoja na kuwapongeza wadau hao alionyesha kuguswa na jitihada zao katika kufanikisha tamasha hilo tangu lilipozinduliwa miaka 9 iliyopita.

“Pamoja na jitihada za wadau wengine wengi katika kufanikisha tamasha hili na kwa kuwa siku ya leo ni maalum kwa ajili ya NBC na TTCL nitumie fursa hii kuwashukuru sana na kuwapongeza kwa jitihada zao katika kufanikisha tamasha hili tangu lilipoanzishwa.’’

“Pamoja na jitihada nyingine nyingi leo hii wadau hawa wawili wametuandalia matukio makubwa matatu muhimu katika kufanikisha tamasha hili ukiwemo uzinduzi huu wa utalii wa kasa hapa Kizimkazi. Pamoja na hili pia wametuandalia mashindano ya mpira kwa vijana na zaidi pia leo wameratibu tamasha kubwa la burudani huko Paje…naahidi kushiriki,’’ alisema Rais Samia kabla ya kushiriki tamasha hilo baadae jioni.

Awali akizungumza kwenye uzinduzi huo Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi alisema tangu kuanzishwa kwa tamasha hilo miaka tisa iliyopita benki ya NBC imekuwa ikitumia vema fursa hiyo si tu kuandaa matukio ya michezo na burudani bali pia kufanikisha jitihada zake mbalimbali za kusaidia jamii hususani katika nyanja za elimu, afya, utalii, michezo na hata huduma za kifedha.

“Tangu kuanza kwa tamasha hili, tulianza kwa kushiriki ujenzi wa madarasa, baadaye tukataoa msaada wa gari la wagonjwa yaani NBC Mobile Clinic ambalo linaendelea kutoa huduma bora za afya, kisha tukashiriki ujenzi na ununuzi wa samani za Saccoss ya Kizimkazi. Baadaae tuliendelea kushiriki ujenzi wa Kituo cha Afya na maeneo mengine ya muhimu ya maendeleo kwa wana-Kizimkazi.’’

“Kifupi, naweza kusema kuwa “sisi Benki ya NBC tumekuwa pamoja na wana-Kizimkazi toka wakati wakisema ‘kizimkazi inakuita’ mpaka leo mwaka 2024 tunaposema “Kizimkazi imeitika”. Aliongeza.

Akizungumzia ushiriki wa benki ya NBC kwenye uzinduzi wa Pango la Salaam (Salaam Cave), Sabi alisema benki hiyo ina nia thabiti ya kukuza utalii nchini na mfanikio ya mradi huo yatasaidia kuzalisha ajira na kuongeza pato la taifa kupitia utalii.

“Benki ya NBC tumejipanga ili kuweka mfumo wa maalum wa malipo ya kidijitali ili kurahisisha malipo ya watalii kwenye pango hilo na maeneo mengine kama haya hapa visiwani Zanzibar,’’ alibainisha.



Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi akizungumza mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan (katikati meza kuu) kuhusu ushiriki wa benki hiyo kwenye Tamasha la Kizimkazi Zanzibar wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa mradi wa utalii wa Samaki aina ya Kasa uliopo kwenye Pango la Salaam (Salaam Cave) katika Shehia ya Kizimkazi Mkunguni uliodhamininiwa pia na benki ya NBC kwa ushirikiano na TTCL, Wadau hao wawili walishirikiana kwa kuandaa matukio kadhaa ya kimichezo, burudani na utalii visiwani humo yaliyohusisha uwepo wa viongozi wakuu wa nchi wakiongozwa na Rais Samia na Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan (wanne kulia) akitazama watalii wakifurahia utalii wa kasa wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa mradi wa utalii wa Samaki aina ya Kasa uliopo kwenye Pango la Salaam (Salaam Cave) katika Shehia ya Kizimkazi Mkunguni uliodhamininiwa pia na benki ya NBC kwa ushirikiano na TTCL.




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan (katikati walioketi) pamoja na viongozi wengine waandamizi wa serikali (walioketi) wakiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa benki ya NBC wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Theobald Sabi (Katikati waliosimama) wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa mradi wa utalii wa Samaki aina ya Kasa uliopo kwenye Pango la Salaam (Salaam Cave) katika Shehia ya Kizimkazi Mkunguni uliodhamininiwa pia na benki ya NBC kwa ushirikiano na Kampuni ya Mawasiliano ya TTCL.




Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango (Katikati) akikabidhi hundi ya zawadi ya pesa taslimu 1.5 Milioni kwa nahodha wa timu ya Shule ya Sekondari Kusini iliyopo Zanzibar baada timu hiyo kuibuka mabingwa wa ligi ya soka ya Vijana wa Kizimkazi ijulikanayo kama “Samia Kizimkazi Youth Cup” kwa kuifunga Shule ya Sekondari Muyuni jumla ya magoli 3-0. Mechi hiyo ilichezwa kwenye Uwanja wa New Amaan Complex mwishoni mwa wiki. Wanaoshuhudia ni pamoja na Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Zanzibar Tabia Maulid (kushoto kwa Makamu wa Rais), viongozi waandamizi wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya, Theobald Sabi (wa tatu kulia). Mashindano hayo yalidhaminiwa na Benki ya NBC kwa kushirikiana na TTCL.




Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango (Katikati) akikabidhi kikombe cha ubingwa kwa nahodha wa timu ya Shule ya Sekondari Kusini iliyopo Zanzibar baada timu hiyo kuibuka mabingwa wa ligi ya soka ya Vijana wa Kizimkazi ijulikanayo kama “Samia Kizimkazi Youth Cup” kwa kuifunga Shule ya Sekondari Muyuni jumla ya magoli 3-0. Mechi hiyo ilichezwa kwenye Uwanja wa New Amaan Complex mwishoni mwa wiki. Wanaoshuhudia ni pamoja na Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Zanzibar Tabia Maulid (kushoto kwa Makamu wa Rais), viongozi waandamizi wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya, Theobald Sabi (wa tatu kulia). Mashindano hayo yalidhaminiwa na Benki ya NBC kwa kushirikiana na TTCL.




Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango (wa pili kushoto) akishuhudia Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya NBC Theobald Sabi (wa pili kulia) akikabidhi ‘kiatu cha dhahabu’ kwa mwanafunzi kutoka Shule ya Sekondari Muyuni ambae aliibuka mfungaji bora kwenye wa ligi ya soka ya Vijana wa Kizimkazi ijulikanayo kama “Samia Kizimkazi Youth Cup” wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi baada ya kukamilika kwa mchezo wa fainali ya ligi hiyo iliyohusisha timu za Sekondari Kusini na Shule ya Sekondari Muyuni.Mechi hiyo ilichezwa kwenye Uwanja wa New Amaan Complex mwishoni mwa wiki ambapo timu ya Sekondari Kusini iliibuka na ushindi wa goli 3-o. Mashindano hayo yalidhaminiwa na Benki ya NBC kwa kushirikiana na TTCL.




Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya NBC wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Theobald Sabi wakifuatia fainali ya ligi ya soka ya Vijana wa Kizimkazi ijulikanayo kama “Samia Kizimkazi Youth Cup” iliyochezwa kwenye Uwanja wa New Amaan Complex mwishoni mwa wiki.









Muonekano wa kikombe cha Bingwa ligi ya soka ya Vijana wa Kizimkazi ijulikanayo kama “Samia Kizimkazi Youth Cup”




Wachezaji wat imu ya Shule ya Sekondari Kusini na Shule ya Sekondari Muyuni zilizopo Zanzibar wakiingia uwanjani kwa ajili ya fainali ya ligi ya soka ya Vijana wa Kizimkazi ijulikanayo kama “Samia Kizimkazi Youth Cup” iliyochezwa kwenye Uwanja wa New Amaan Complex mwishoni mwa wiki. Mashindano hayo yalidhaminiwa na Benki ya NBC kwa kushirikiana na TTCL.






Wachezaji wa Shule ya Sekondari Kusini iliyopo Zanzibar wakifurahia pamoja na uongozi wa timu hiyo baada timu hiyo kuibuka mabingwa wa ligi ya soka ya Vijana wa Kizimkazi ijulikanayo kama “Samia Kizimkazi Youth Cup” kwa kuifunga Shule ya Sekondari Muyuni jumla ya magoli 3-0. Mechi hiyo ilichezwa kwenye Uwanja wa New Amaan Complex mwishoni mwa wiki. Wanaoshuhudia ni pamoja na Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Zanzibar Tabia Maulid (kushoto kwa Makamu wa Rais), viongozi waandamizi wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya, Theobald Sabi (wa tatu kulia). Mashindano hayo yalidhaminiwa na Benki ya NBC kwa kushirikiana na TTCL.

About life goes on

Blogger | Journalist | Entrepreneur | Fashonista Based in Dar es Salaam, Tanzania.

0 comentários :

Post a Comment