DASH COMMUNICATION

DASH COMMUNICATION

ZANELLE BONGO LADIES WEAR

ZANELLE BONGO LADIES WEAR

ANDY BEACH

ANDY BEACH

AK

AK

NASAROG

NASAROG

NAKEMEA MAUAJI YA ALBINO

NAKEMEA MAUAJI YA ALBINO

Baby shop

Baby shop

COCO BEACH

COCO BEACH

RJ

RJ

Home » » SAKATA LA MAUAJI YA SWETU FUNDIKIRA

SAKATA LA MAUAJI YA SWETU FUNDIKIRA

         Naanza kwa kuwapa pole familia ya marehemu Swetu Fundikira na wote walio guswa na msiba huu kwa namna moja au nyingine.
          Kesi ya mauaji ya Swetu Fundikira iliyotingisha mji kwa takribani miaka miwili imeisha jana na wanajeshi wote watatu wamepatikana na hatia na wote wamehukumiwa KUNYONGWA MPAKA KUFA.


      HAWA NDIO WANAJESHI WALIOMUUA MTOTO WA CHIEF FUNDIKIRA.

      Nijambo lakusikitisha sana kuona watu tunaowategemea kutulinda hili hali wenyewe wanatumia madaraka hayo kwa kutuangamiza. Sijawahi kuhudhuria KESI yeyote mahakamani na hii ndio kesi ya kwanza na ninapenda kuchukua nafasi hii kuipongeza mahakama na JAJI wake kwakuendesha kesi hii kwa ufasaha wa hali ya juu. Step by step bila papara japo kesi ilijionesha tokea mwanzo iko wazi nawana hatia lakini iliendesha kwa mtiririko ikitaka wenyewe watuhumiwa wajielezee mpaka watakapo kwama na kukiri kosa.
      Sasa basi mambo yalikuwa hivi........Marehemu Swetu Fundikira alikuwa abiria tu kwenye gari dogo pamoja na wenzake wakitokea matembezini mwao gafla walitaka kugongana na gari nyingine ndogo ambayo ilikuwa na wanajeshi (watuhumiwa) watatu nao vile vile walikuwa wakitokea kwenye matembezi yao. tukio hili limetokea pale junction ya kwenda mwananyamala ukitokea kinondoni. Katika ugomvi Wanajeshi walitaka watambulike wenyewe ni wakina nani katika juhudi za kuoneshana ubabe walifanikiwa kumchukua marehemu Swetu wakidai kuwa wanaenda naye kituoni kwa maelezo zaidi. Hapa tu tunaona utata wa tukio kumbuka Marehemu hakuwa dereva kwahiyo hakustahili kuchukuliwa yeye hatakama walifanyiwa fujo barabarani wangepaswa kumchukua dereva aliyehusika na tukio hilo. (HII YOTE NI ISHARA YA MTU KUTAKA KUONYESHA UBABE) sitaki kuhukumu sana maana tayari mahakama yetu tukufu imeshatenda haki yao ila hebu ona sasa wakamchukua mtu wa watu masikini na yeye labda baada yakuona wamejitambulisha ni wanajeshi akajua yuko kwenye mikono salama na kukubali kuingia kwenye gari kumbe anajiingiza kwenye mikono ya MAJAMBAZI tena hatari... watu walitegemea anapelekwa kituo cha Oysterbay Police maana ndicho kilikuwa karibu na eneo hilo lakini wapi Salender Bridge Police Post nako wakapitiliza sasa huko kwingine walikuwa wanaelekea wapi na walikuwa wanania gani? hapo ni tosha kabisa kujua hawa watu hawakuwa na nia nzuri kabisaaaaa. Haitoshi hiyo marehemu amekutwa ufukweni wa bahari na akiwa mtupu kabisaa na huku akiwa anamajeraha makubwa kichwani tu na si kwingine labda useme anamichuruzo ya kupigana huku na kule na kwa ujinga wao wanazidi kudanganya eti nguo zilivuka pale junction ya mwananyamala wakati wa ugomvi na waliomvua nguo walikuwa ni raia wa kinondoni dah!! uongo mwingine bwana ikumbukwe kuwa marehemu alikuwa anaishi kinondoni hiyo hiyo ni mwenyekiti wa club ya mpira kitu ambacho vijana wengi wanamfahamu si hivyo tu alikuwa Diwani wa kata hiyo sasa wananchi wake wamemrarua nguo na kumuacha mtupu???
       Hii yote inaonesha kwamba Wanajeshi hawa watatu walitaka kumuonesha ubabe marehemu ili akasimulie wenzake sasa tujifunze watu wote HASIRA NI HASARA katika piga piga na hasira zao na mafunzo yao ya uwanajeshi walijikuta wamemuumiza marehemu na kuona wameharibu changanya na pombe walizo kunywa wakajikuta wanaamuwa maamuzi potofu kabisaa kwamba labda wakamtose baharini kupoteza ushahidi, kumbuka tena mtu akifa akavuliwa ngu na kutoswa baharini kuja kuibuka na kugundulika itachukua muda mrefu sana hapo kuja kugundua tukio zima tena basi ushahidi hamna ukizingatia atakuwa ameliwa na samaki labda au kaharibika nivigumu kujua majeraha nakubakia tu labda alilewa akadumbukia baharini. JIULIZE BAHARINI WALITAFUTA NINI? NGUO WALIMVUA ZA NINI? KICHWANI KUBONDWA INAJULIKANA KABISA ILI UFE HARAKA sasa kuna la nyongeza yoyote juu ya nani kaua? mtu alikuwa mzima umeonekana kabisa unaondoka naye badala ya kukutwa kituoni unakutwa na mtu mahututi mtupu halafu muda kidogo anafariki je unaelezea nini walimwengu wakuelewe?
        Damu ya Kichief ilivyokuwa na nguvu..... maana si jambo la kawaida mpita njia tena dereva tax atumie nguvu zake mafuta yake na muda wake baada ya kuona tukio kwambali watu wakimpiga mwenzao akaenda kuripoti taarifa kituo cha salender. Hapo sasa uone damu nzito mara doria wakafika eneo latukio hamadi na kuwakuta washtakiwa wanajeshi wote watatu wakiwa na marehemu katika hali mbaya hajitambui pia akiwa mtupu bila nguo. 
        Kesho yake Swetu Fundikira aliaga dunia ni jambo la kusikitisha kwa kweli mtu kukatishwa uhai gafla. Marehemu ameacha wake wawili na watoto hili hali mke mdogo akiwa mjamzito this is very sad, maana baby SIVUNO amezaliwa hakiwa hamjui baba amepotezewa haki yake ya kuita baba.
        Kesi iliendelea na ushahidi ulitolewa japo kulikuwa na uongo wa kitoto na kutunga huku na kule kwa upande wa mashahidi. mtu anaulizwa imekuaje umekutwa na Swetu akiwa hajitambui wakati umeondoka naye mzima anajibu liliuwa jambazi na alikuwa anajitetea asidhuriwe hivi wewe mwanajeshi kamili tena watatu mnashindwa kumzibiti jambazi bila ya kumuua? ni mafunzo ya wapi mlifundishwa kukamata waalifu na kuwauwa? na hii si kwa hawa tu vitendo hivi vinafanyika kote duniani POLICE, WANAJESHI, WAGAMBO NA VIONGOZI waliowekwa kulinda na kutetea mali na watu lakini wenyewe wanatumia madaraka hayo kuwanyonga na kuwadhurumu na kuwadidimiza na hata kuwahua raia wasio na kosa.
Sasa hii ni fundisho kwa wote wenyekuonea wanyonge nakujichukulia sheria mkononi. Kumbuka Hasira ni Hasara dhibiti hasira zako kijana zitakuponza.
         Mambo yalivyoenda mahakamani jana maana ndugu wa wanajeshi waliohukumiwa kunyongwa walilia na wa marehemu Swetu walitoka mahakamani hili hali wakilia na wengine kuzirai hii ni furaha pamoja na uzuni msiba ulianza upyaa maana wengi wao wali valia mavazi meusi wakiashiria msiba.
Dada wa marehemu akilia kuwa sasa amemzika kwa amani kaka yake.

Dada wa marehemu Mwasiti na Rehema walizimia kabisaa


Wadogo wa marehemu pichani (Mkala Fundikira anaye bembelezwa na kaka yake)

Media ilitawala mahakamani nikiwa mmojawapo ahaaaa

Binti wa marehemu Misuka Swetu Fundikira akiwa na mama yake Lucy Njeri (mama Sivuno)

Mahakama kuu ilifurika jana

Jeedygirl mwenyewe nikiwa nimelowa jasho harakati za kupiga picha 



REST IN PEACE BABU SWETU FUNDIKIRA WE WILL    
                                            ALWAYS MISS U

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by : Jeedy Girl
Copyright © 2012. life goes on - All Rights Reserved
Modified by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Jeedy Girl