DASH COMMUNICATION

DASH COMMUNICATION

ZANELLE BONGO LADIES WEAR

ZANELLE BONGO LADIES WEAR

ANDY BEACH

ANDY BEACH

AK

AK

NASAROG

NASAROG

NAKEMEA MAUAJI YA ALBINO

NAKEMEA MAUAJI YA ALBINO

Baby shop

Baby shop

COCO BEACH

COCO BEACH

RJ

RJ
Home » » SUGU UMECHEMSHA MRUDISHE SASHA

SUGU UMECHEMSHA MRUDISHE SASHA


Nimefuatilia sakata la mh. Sugu kumnyanganya mtoto aliyekuwa mke wake Faiza kwakweli nimeshindwa kuelewa sababu kuu na nashangaa hiyo sheria iliyotumika kufikia maamuzi hayo
Kwanza kabisa mavazi si sababu ya mtu kushindwa kulea mtoto naomba itambulike kuwa kunawatu wana vaa mashungi kutwa lakini ni wazinzi na wengine wanatesa watoto lakini hawajawahi kushukuliwa sheria ya kunyang'anywa watoto wao.
Pili haka katoto bado ni kadogo kanaitaji mapenzi ya mama yake na malezi ya mama jamani atalelewaje na mama wa kambo wakati mama mzazi yuko na anajiweza?
 
Tatu tukianza kuhesabiana maovu jamani nani asiye jua Sugu alikuwa kwenye muziki tena wazamani wa kihuni wa mabangi na uovu kibao kama kijana kapitia na kufanya kama sasa kawa muheshimiwa na kabadilika basi angepaswa kumrekebisha mzazi mwenzie na kuwekana sawa kwa faida ya mtoto wao na siyo kukomoana.
Siingilii kazi ya mahakama lakini this is not fair ingekuwa binafsi ohoooo hata sielewi naongea kama mzazi mama wa watoto wawili jamani watoto wanauma asikueleze mtu unakesha unaangaika naye mtu hana msaada na wewe anakutelekeza leo mtoto kamekuwa kidogo anakuja ninyakulia mwanangu eti kisa nimetoka disco nimevaa kaptula sijui nini hell no.
Nashauri kwamba kama alikuwa namkomoa huyo mama wa watu basi atakuwa amejikomoa na yeye na bahati mbaya amelenga siku mbaya kabla ya uchaguzi kama alifikiria sakata hili litampa kiki ya kupata kura nahisi kanoa kapotea kabisaaa angetafuta kitu kingine si kumpa mateso mtoto maana hapa anachezea maisha ya mtoto.
NANI KAKUAMBIA MTOTO NI WAMAMA WA KAMBO..... MTOTO KWA MAMA BWANA ACHA KUMFANYA MTOTO AKATESEKE BURE WAKATI MAMA YAKE YUPO NA ANAMPENDA NA KUMJALI MAVAZI HAYA LEI FAHAMU.
 
Pichani mtoto akifurahia maisha na mama yake

Mama yake hakushindwa kumsomesha na kumvisha muone alivyo pendeza

Faiza aliweza kupata muda wa kufanya homework na mwanaye sasa sijui nilipi ambalo limefanya mama huyu kunyang'anywa mtoto wakati malezi yote kama mama anampatia mwanaye.

 

Wakiwa pamoja kama familia Sugu, Faizal na Baby Sasha


Joseph Mbilinyi maarufu kwa jina la Sugu


Mavazi yanayosemekana kumponza Faiza Allyhadi kunyang'anywa mtoto wake na Sugu.

HAKI YA MAMA NA MTOTO IKO WAPI TUNAOMBA WANASHERIA MTUSAIDIE KUHUSU HILI KAMA AMEKOSEA KUVAA MAVAZI YASIYOSTAHILI LIANGALIWE AMEVAA WAPI NAKAMA HIVYO WAMAMA WOTE WANAOTOKA DISCO USIKU NA MAVAZI YAO WAKAMATWE NA KUNYANG'ANYWA WATOTO TUJUE MOJA HIYO SHERIA IPO KULIKO KUMNYANYASA MAMA SASHA WA WATU.
MUHIMU APEWE ONYO AKIRUDIA NDIO ACHUKULIWE HATUA NA SI KUNYANG'ANYWA MTOTO.

HII NI DUNIA YETU ZAIDI UIJUAVYO.......LIFE GOES ON.....

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by : Jeedy Girl
Copyright © 2012. life goes on - All Rights Reserved
Modified by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Jeedy Girl