DASH COMMUNICATION

DASH COMMUNICATION

ZANELLE BONGO LADIES WEAR

ZANELLE BONGO LADIES WEAR

ANDY BEACH

ANDY BEACH

AK

AK

NASAROG

NASAROG

NAKEMEA MAUAJI YA ALBINO

NAKEMEA MAUAJI YA ALBINO

Baby shop

Baby shop

COCO BEACH

COCO BEACH

RJ

RJ

Home » » BALOZI WA PSPF MWANAMITINDO WA KIMATAIFA FLAVIANA MATATA AKABIDHI MABEGI NA MADAFTARI KWA SHULE ZA MSINGI DODOMA NA SINGIDA

BALOZI WA PSPF MWANAMITINDO WA KIMATAIFA FLAVIANA MATATA AKABIDHI MABEGI NA MADAFTARI KWA SHULE ZA MSINGI DODOMA NA SINGIDA

Balozi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Flaviana Matata, ametoa wito kwa wanafunzi wa shule za msingi Chididimo iliyoko Manispaa ya mji wa Dodoma na ile ya Nyerere iliyoko mkoani Singida kuwahimiza wazazi wao kujiunga na Mfuko huo.
Balozi huyo ambaye pia ni Mwanamitindo wa Kimataifa anayefanyia kazi zake nchini Marekani, ameyasema hayo kwa nyakati tofauti, wakati akikabidhi vifaa vya shule kwa wanafunzi hao Oktoba 7, 2015.
 
“Mimi kama Balozi wa PSPF, ninatoa wito kwa wanafunzi mliopo hapa, kufikisha ujumbe huu kwa wazazi wenu, kwani kujiunga na PSPF kuna faida nyingi katika maisha ya sasa na ya baadae."
Alisema, PSPF inatoa mikopo mbalimbali kwa wanachama wake kama vile ya viwanja, mkopo wa elimu, na mkopo wa kuanzisha maisha.
Lakini pia PSPF inatoa mafao mbalimbali kwa wanachama wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari, yaani (PSS), ikiwemo, Fao la Uzazi, Fao la Uzeeni, Fao la Elimu, Fao la Ulemavu na Fao la Ujasiriamali.
“Wazazi wenu wawe wakulima, wafanyakazi walioajiriwa au kujiajiri wanaweza kujiunga na PSPF kupitia mpango wa Uchangiaji wa Hiari.” Alifafanua Balozi huyo.
 
Naye Afisa Masoko Mwandamizi wa PSPF, Rahma Jemina Ngassa, alisema moja ya Sera za Mfuko huo ni kuchangia sekta ya Elimu na msaada huo ni utekelezaji wa Sera wa kusaidia jamii.
 
 PSPF inaamini vifaa hivyo vitapunguza kwa kiasi Fulani changamoto zilizokuwa zinawakabili wanafunzi hao na hivyo watakuwa kwenye nafasi nzuri ya ushiriki wa masomo kikamilifu.
Kwa upande wake, Kaimu Afisa Elimu Manispaa ya Dodoma, Christopher Ligonda, ameupongeza Mfuko huo kwa kuwajali wanafunzi ambao wazazi wao kwa namna moja au nyingine ni wanachama au wanachama watarajiwa na hata wanafunzi wenyewe.
Naye Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Nyerere iliyoko mkoani Singida, Yesaya Ramadhani, ameushukuru uongozi wa PSPF kwa kuwafikiria wanafunzi wa shule hiyo katika kuwasaidia vifaa hivyo ambavyo ni mabegi na madaftari kuwa ni kitendo cha kweli katika kusaidia jamii ambayo inakabiliwa na changamoto mbalimbali.
 

 Balozi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Flaviana Matata, na Afisa Masoko Mwandamizi wa Mfuko huo, wakiwa katikati ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Nyerere, wakati walipofika kutoa msaada wa mabegi na madaftari kwa baadhi ya wanafunzi hao wenye mahitaji maalum Oktoba 7, 2015.
 
 
Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw.Said akikabidhi begi kwa mwanafunzi wa Shule ya Msingi Nyerere iliyoko mkoani Dodoma Oktoba 7, 2015.
 
Flaviana akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya walimu wa Shule ya Msingi Nyerere, akiwemo Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Yesaya Ramadhani (katikati), baada ya kukabidhi msaada huo. Kulia ni Afisa Masoko Mwandamizi wa Mfuko huo, Rahma Jemina Ngassa
 
 
 Kaimu Afisa Elimu wa Manispaa ya Dodoma, Christopher Legonda, (kushoto), akitoa shukrani zake baada ya Mfuko wa  Pensheni wa PSPF, kutoa msaada wa mabegi na madaftari kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Chididimo iliyokonje kidogo ya Manispaa hiyo Oktoba 7, 2015. Wakwanza kulia ni Balozi wa PSPF, Flaviana Matata, na katikati ni Afisa Masoko Mwandamizi wa Mfuko huo, Rahma Jemina Ngassa.
 
 Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Chididimo iliyoko nje kidogo ya Manispaa ya Dodoma, Bright P. Mzava, akizungumza kwenye hafla hiyo ya kupokea msaada wa vifaa vya Shule kwa wanafunzi wa Shule hiyo Oktoba 7, 2015
 
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Chididimo, Keneth Henry (kulia) na Marina Hamisi, wakisoma risala
 
 Flaviana akipiga picha mwenyewe, “Selfie” na wanafuzni wa Shule ya Msingi Chididimo
 
PSPF kupitia Sera yake ya kusaidia jamii imetoa msaada wa mabegi na madaftari kwa shule ya Nyerere iliyoko Singida na ile ya Chididimo iliyoko nje kidogo ya Manispaa ya Dodoma
 

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by : Jeedy Girl
Copyright © 2012. life goes on - All Rights Reserved
Modified by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Jeedy Girl