Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) umeanza kupokea wageni waliojumuika katika ofa maalumu ya Sabasaba kwa kutembelea vivutio vya utalii vinavyosimamiwa na wakala huo. Safari ya kwanza imewapeleka wageni hao katika Magofu ya Kaole yaliyopo wilayani Bagamoyo.
Wageni hao, wakiwemo Watanzania na raia wa kigeni, walipata fursa ya kutembelea eneo hilo la kihistoria na kujifunza kuhusu historia ya ustaarabu wa pwani ya Afrika Mashariki pamoja na urithi wa kihistoria wa Tanzania.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mhifadhi Mambo Kale Daraja la II, Veronica Kombe, aliwahamasisha wananchi kutumia ofa ya Sabasaba kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii vinavyosimamiwa na TFS. Alibainisha kuwa safari inayofuata itafanyika Julai 11 kuelekea Msitu wa Asili wa Pugu–Kazimzumbwi.
Baadhi ya wageni walioshiriki ziara hiyo walieleza kufurahishwa na uzoefu walioupata, wakisema wamefanikiwa kujionea kwa karibu maeneo ambayo kwa muda mrefu walikuwa wakiyasikia kupitia simulizi na kusoma kwenye vitabu.
Kupitia ofa hiyo ya Sabasaba, TFS inalenga kuwapa wananchi fursa ya kutembelea vivutio vya utalii kwa gharama nafuu, kujifunza historia, kuhamasisha utalii wa ndani, na kuongeza uelewa kuhusu umuhimu wa kuhifadhi urithi wa asili na kihistoria wa Tanzania.
.jpeg)
.jpeg)


.jpeg)

0 comentários :
Post a Comment