EWURA YASHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

MWENYEKITI   wa Wanawake wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya Tanzania (TUGHE) Tawi la EWURA, Herieth Kasilima, akiwaongoza baadhi ya Wafanyakazi Wanawake wa EWURA  waliojitokeza katika maadhimisho ya  kilele cha Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika   ngazi ya Mkoa wilayani Kongwa ,mkoani Dodoma Machi 8,2026 wakipita mbele ya mgeni rasmi wa maadhimisho hayo ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Staki Senyamule.

....

WAFANYAKAZI wanawake wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) leo 8 Machi 2026, wameungana na wanawake wengine kutoka maeneo mbalimbali kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika ngazi ya Mkoa  wilayani Kongwa mkoa wa Dodoma.

Maadhimisho hayo yalifunguliwa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Staki Senyamule, na kusisitiza kuwa Serikali itaendelea kuwawezesha wanawake na wasichana katika nyanja mbalimbali ili kuhakikisha usawa wa kijinsia na ustawi wa wanawake nchini.

Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo, Mwenyekiti wa Wanawake wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya Tanzania (TUGHE) Tawi la EWURA, Herieth Kasilima, aamesema  kuwa kaulimbiu ya maadhimisho hayo ambayo ni “Haki na usawa kwa wanawake na wasichana,” inalenga kuhamasisha jamii kuhakikisha wanawake na wasichana wanapata haki na fursa sawa katika nyanja mbalimbali za maisha, jambo ambalo pia linaendana na malengo ya maendeleo ya kimataifa kuelekea mwaka 2030 na ajenda ya maendeleo ya mwaka 2050.

Aidha, ametumia fursa hiyo kuwahimiza wanawake wanaojihusisha na kazi za ufundi umeme kujitokeza kujisajili na kupata leseni kupitia mifumo ya EWURA ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi na kwa mujibu wa sheria.

Alifafanua kuwa kwa mujibu wa sheria na kanuni za EWURA, mafundi umeme wanapaswa kuwa na leseni rasmi ili kufanya shughuli zao hali itakayowapelekea kuepuka changamoto au usumbufu katika utekelezaji wa kazi zao.

“Wanawake wote wanaofanya kazi za ufundi wa umeme, hususan wale wasio na leseni za EWURA wajitokeze kujisajili EWURA ili waweze kufanya shughuli zao kwa ufanisi,na bila usumbufu wowote,” alisisitiza.

Maadhimisho hayo yamekuwa jukwaa muhimu la kuwakutanisha wanawake kutoka sekta mbalimbali kujadili masuala ya usawa wa kijinsia, haki za wanawake pamoja na mchango wao katika maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla.

Wafanyakazi wanawake wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) wakiwa katika maandamano walipoungana na wanawake duniani kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani  Machi 8,2026  ambapo mkoani Dodoma maadhimisho hayo yenye kauli mbiu “Haki na usawa kwa wanawake na wasichana,”yamefanyika katika Wilaya ya Kongwa.

MWEYEKITI   wa Wanawake wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya Tanzania (TUGHE) Tawi la EWURA, Herieth Kasilima, akiwaongoza baadhi ya Wafanyakazi Wanawake wa EWURA  waliojitokeza katika maadhimisho ya  kilele cha Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika   ngazi ya Mkoa wilayani Kongwa ,mkoani Dodoma Machi 8,2026 wakipita mbele ya mgeni rasmi wa maadhimisho hayo ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Staki Senyamule.

Wafanyakazi wanawake wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) wakiwa katika Picha ya pamoja mara baada ya kushiriki Maadhimisho  Siku ya Wanawake Duniani Machi 8,2026 ambapo mkoani Dodoma maadhimisho hayo yenye kauli mbiu “Haki na usawa kwa wanawake na wasichana,”yamefanyika katika Wilaya ya Kongwa.

About Judith Mwaheleja

I am a Tanzanian Blogger , Entrepereneur and Fashonista.

0 comentários :

Post a Comment