NIDHAMU YA KIFEDHA YAWALIPA WAKULIMA; EFTA YAREJESHA TAKRIBANI SHILINGI MILIONI 100, YAFIKIA NPL YA ASILIMIA 1


WhatsApp%20Image%202026-08-07%20at%2019.36.43
Mkurugenzi Mtendaji wa EFTA Bw Nicomed Bohay akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha wakati wa hafla ya kukabidhi hudhi za rejesho la asilimia hamsini.
WhatsApp%20Image%202026-08-07%20at%2019.35.37
Mkurugenzi Mtendaji wa Equity for Tanzania Limited (EFTA), Bw. Nicomed Bohay (kushoto), akimkabidhi Bi. Elimiti Mushi hundi ya rejesho la asilimia 50 ya riba kwa niaba ya mume wake, Bw. Elimiti Mushi (katikati), mmoja wa wakulima 37 walionufaika na Mpango wa EFTA wa Urejeshaji wa Asilimia 50 ya Riba (Interest Rebate Programme) baada ya kurejesha mkopo wake wa mashine za kilimo kwa wakati na kwa kuzingatia nidhamu ya kifedha. Kupitia mpango huo, EFTA imerejesha takribani Shilingi milioni 100 kama rejesho la riba kwa wakulima wanaotekeleza kwa uaminifu wajibu wao wa kurejesha mikopo kwa wakati.
WhatsApp%20Image%202026-08-07%20at%2019.35.36
Mkurugenzi Mtendaji wa Equity for Tanzania Limited (EFTA), Bw. Nicomed Bohay (kushoto), akimkabidhi Bw. Lawei Akonaay wa Babati, Mkoa wa Manyara (kulia), hundi ya rejesho la asilimia 50 ya riba baada ya kukamilisha marejesho ya mkopo wake wa mashine za kilimo kwa wakati na kwa kuzingatia masharti ya mkataba.
WhatsApp%20Image%202026-08-07%20at%2019.35.36%20(1)
Mkurugenzi Mtendaji wa Equity for Tanzania Limited (EFTA), Bw. Nicomed Bohay (kushoto), akimkabidhi Bw. Sebastian Gwaltu wa Gehandu, Mkoa wa Manyara (kulia), hundi ya rejesho la asilimia 50 ya riba baada ya kukamilisha marejesho ya mkopo wake wa mashine za kilimo kwa wakati na kwa kuzingatia masharti ya mkataba.
WhatsApp%20Image%202026-08-07%20at%2019.35.36%20(2)
Mkurugenzi Mtendaji wa Equity for Tanzania Limited (EFTA), Bw. Nicomed Bohay (kushoto), akimkabidhi Bw. Pascali Gwasma wa Katesh, Mkoa wa Manyara (kulia), hundi ya rejesho la asilimia 50 ya riba baada ya kukamilisha marejesho ya mkopo wake wa mashine za kilimo kwa wakati na kwa kuzingatia masharti ya mkataba.
WhatsApp%20Image%202026-08-07%20at%2019.35.35
Mkurugenzi Mtendaji wa Equity for Tanzania Limited (EFTA), Bw. Nicomed Bohay (kushoto), akimkabidhi Bw. Patrice Boay wa Katesh, Mkoa wa Manyara (kulia), hundi ya rejesho la asilimia 50 ya riba baada ya kukamilisha marejesho ya mkopo wake wa mashine za kilimo kwa wakati na kwa kuzingatia masharti ya mkataba.
WhatsApp%20Image%202026-08-07%20at%2019.35.34

WhatsApp%20Image%202026-08-07%20at%2019.35.34%20(1)

WhatsApp%20Image%202026-08-07%20at%2019.35.34%20(2)

WhatsApp%20Image%202026-08-07%20at%2019.35.33
Mkurugenzi Mtendaji wa Equity for Tanzania Limited (EFTA), Bw. Nicomed Bohay (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa wakulima walionufaika na Mpango wa EFTA wa Urejeshaji wa Asilimia 50 ya Riba (Interest Rebate Programme) baada ya hafla ya kukabidhi hundi za rejesho la asilimia 50 ya riba iliyofanyika wakati wa Maonesho ya Nanenane 2026 jijini Arusha. Kupitia mpango huo, EFTA imerejesha takribani Shilingi milioni 100 kama rejesho la riba kwa wakulima 37, ikiwa ni kutambua nidhamu yao ya kifedha na marejesho ya mikopo kwa wakati.
WhatsApp%20Image%202026-08-07%20at%2019.35.33%20(1)
Mkurugenzi Mtendaji wa Equity for Tanzania Limited (EFTA), Bw. Nicomed Bohay (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa EFTA kutoka Matawi ya Arusha na Moshi wakati wa hafla ya kukabidhi hundi za rejesho la asilimia 50 ya riba kwa wakulima walionufaika na Mpango wa EFTA wa Urejeshaji wa Asilimia 50 ya Riba (Interest Rebate Programme), iliyofanyika katika Maonesho ya Nanenane 2026 jijini Arusha. Kupitia mpango huo, EFTA imerejesha takribani Shilingi milioni 100 kwa wakulima 37 ikiwa ni kutambua nidhamu yao ya kifedha na marejesho ya mikopo kwa wakati.


Na Mwandishi wetu, Arusha


Equity for Tanzania Limited (EFTA) imewarejeshea wakulima 37 takribani Shilingi milioni 100 kama sehemu ya mpango wake wa Interest Rebate Programme, unaolenga kuwazawadia wateja wanaorejesha mikopo yao kwa wakati na kwa kufuata masharti ya mikataba yao.


Mpango huo, ambao umefanyika kwa miaka miwili mfululizo, umehusisha kurejeshwa kwa Shilingi milioni 43 kwa wakulima 15 mwaka 2025 na Shilingi milioni 53 kwa wakulima 22 mwaka 2026, na kufikisha jumla ya takribani Shilingi milioni 100 kwa wakulima 37.


Akizungumza katika hafla ya kukabidhi fedha hizo iliyofanyika kwenye banda la EFTA wakati wa Maonesho ya Nanenane 2026 jijini Arusha, Mkurugenzi Mtendaji wa EFTA, Bw. Nicomed Bohay, alisema mpango huo ni sehemu ya mkakati wa kampuni wa kujenga utamaduni wa nidhamu ya kifedha kwa wateja wake.


"Interest Rebate Programme ni zaidi ya kurejesha sehemu ya riba kwa wateja wetu. Tunataka kuwajengea wakulima utamaduni wa nidhamu ya kifedha kwa kuwaonyesha kuwa kulipa mkopo kwa wakati kuna manufaa ya moja kwa moja," alisema.


Alisema nidhamu ya marejesho iliyoonyeshwa na wakulima hao imechangia kwa kiasi kikubwa kuimarika kwa utendaji wa kampuni.


Kwa mujibu wa Bw. Bohay, hadi kufikia mwezi Juni mwaka huu, EFTA imefikia kiwango cha asilimia moja (1%) cha mikopo chechefu (Non-Performing Loans – NPL), kiwango ambacho ni miongoni mwa viwango vya chini zaidi katika sekta ya taasisi za fedha nchini.


Alieleza kuwa mafanikio hayo yana uzito mkubwa zaidi kwa kuwa EFTA inajihusisha na ufadhili wa mali zinazohamishika, zikiwemo matrekta, mashine za kilimo, magari ya biashara na vifaa vingine vya uzalishaji ambavyo kwa kawaida hubeba kiwango kikubwa zaidi cha hatari ya mikopo.


"Nidhamu waliyoionyesha wakulima hawa ndiyo imechangia EFTA kufikia kiwango hiki cha NPL. Hii inatuwezesha kuendelea kuwafikia wakulima wengi zaidi kwa huduma za ufadhili wa mashine na vifaa vya uzalishaji," alisema.


Mbali na kuwanufaisha wakulima hao kwa kurejeshewa sehemu ya riba, uwekezaji walioufanya kupitia mashine na vifaa vilivyofadhiliwa na EFTA umechangia kufunguliwa kwa zaidi ya ajira 300.


Ajira hizo zinahusisha madereva wa matrekta, waendesha mitambo, mafundi, waendeshaji wa mashine pamoja na vibarua wanaoshiriki katika shughuli mbalimbali za uzalishaji na uchakataji wa mazao.


Kupitia mashine hizo, wakulima wameongeza uzalishaji, kupunguza gharama za shughuli za kilimo na kuboresha thamani ya mazao yao.


Mmoja wa wanufaika wa mpango huo, Erimiti Mushi kutoka Arusha, alisema mashine aliyopata kupitia EFTA imemwezesha kuongeza uzalishaji na kuwahudumia wakulima wengine wanaohitaji huduma za kilimo cha mashine.

"Fedha tulizorejeshewa ni motisha kubwa kwetu. Zinathibitisha kwamba taasisi hii inathamini wateja wanaorejesha mikopo yao kwa wakati," alisema.


Naye Sebastian Gwaltu kutoka Katesh, mkoani Manyara, alisema ufadhili wa mashine za uzalishaji umemsaidia kuongeza ufanisi katika shughuli zake za kilimo kuanzia maandalizi ya mashamba hadi uchakataji wa mazao.

Alisema fedha alizorejeshewa kupitia mpango huo zitamuwezesha kuendelea kuwekeza katika shughuli zake za uzalishaji.


Mbali na hafla hiyo, EFTA imeendelea kutumia Maonesho ya Nanenane 2026 kuwaelimisha wakulima kuhusu fursa za kupata ufadhili wa matrekta, power tillers, mashine za uchakataji wa mazao na vifaa vingine vya uzalishaji vinavyosaidia kuongeza tija katika kilimo.


Katika maonesho hayo, mamia ya wakulima na wadau wa sekta ya kilimo wameendelea kutembelea banda la EFTA kupata elimu kuhusu huduma za kampuni hiyo na namna zinavyoweza kuwasaidia kukuza shughuli zao za kiuchumi.


Kwa mujibu wa EFTA, mpango wa Interest Rebate unaonyesha kuwa huduma za kifedha zinaweza kuwa zaidi ya utoaji wa mikopo. Kupitia kuhamasisha nidhamu ya marejesho, kampuni imeweza kurejesha takribani Shilingi milioni 100 kwa wakulima 37, kufikia kiwango cha asilimia 1 cha mikopo chechefu (NPL) na wakati huo huo kuchangia kuundwa kwa zaidi ya ajira 300 kupitia uwekezaji wa wakulima hao katika mashine na vifaa vya uzalishaji.

About Judith Mwaheleja

I am a Tanzanian Blogger , Entrepereneur and Fashonista.

0 comentários :

Post a Comment