Wednesday, 28 August 2024

DKT. SAMIA AWATAKA WAKUU WA TAASISI ZA UMMA KUWA WABUNIFU NA KUTOOGOPA MABADILIKO.


Na. Vero Ignatus

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassani amefungua Kikao kazi cha pili cha Wenyeviti wa Bodi ya Watendaji wakuu wa, Taasisi za Umma 2024 ambapo amesema suala la mageuzi ni agenda ngumu lakini mabadiliko yanapokuwepo maendeleo yanatokea uli kulinda rasilimali za wananchi na kutimiza lengo la kuanzishwa kwake

Dkt. Samia ametoa kauli hiyo mapema leo Agosti 28, 2024 wakati akifungua kikaokazi cha Wenyeviti wa bodi na watendaji wakuu wa Taasisi za umma kuendelea kufanya mabadiliko ya kiutendaji ndani ya Taasisi hizo ili kuondokana na utegemezi sambamba na kutokuogopa mabadiliko yanapofanyika

Amesema kuwa serikali inaposisitiza mabadiliko, ufanisi, Mashirika yalete faida ni kulinda rasilimali za wananchi ambazo zimewekezwa ndani ya mashirika hayo lakini pia ni kutengeneza lengo la kuundwa kwa mashirika haya kwahiyo mabadiliko hayo yanafanywa kwa lengo tarajiwa na kwa nia njema kabisa ya kujenga uchumi wa nchi

"Mabadiliko haya tunayafamya kwa nia njema ya kujenga nchi yetu katika maamuzi ya Kiutendaji"

Amewataka Wenyeviti hao kujadiliana kwa upana Kauli mbiu hiyo na kuipa nafasi ili Mashirika mengine yaweze kufanya kuendana na mageuzi hayo yenye kuleta mchango mkubwa katika Taasisi hizo kwaajili ya kuweza kuchangia Pato la uchumi wa Taifa

Tunaposisitiza mabadiliko, ufanisi, Mashirika yalete faida ni kulinda rasilimali za wananchi ambazo zimewekezwa ndani ya mashirika hayo lakini pia ni kutengeneza lengo la kuundwa kwa mashirika haya kwahiyo mabadiliko haya tunayafanya kwa nia njema kabisa ya kujenga nchi yetu." Amenukuliwa Rais Samia.

Akitoa Salam kwa niaba ya mkoa,Mkuu wa mkoa wa Arusha Paul Christian Makonda leo agosti 28.2024 amemkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan na kumshukuru kwa kutoa shilingi Bil 7 kwaajili ya uapanuzi wa uwanja wa ndege Kisongo Arusha kwani ykarabati huo utaondoa changamoto ya wageni kutoka KIA kuelekea Jijini Arusha

Vile vile Makonda alimkaribisha Dkt Samia kwa kumwambia kwamba mwezi wa 10 mkoa wa Arusha unakwenda kuvunja rekodi ya Guinness iliyowekwa na Ujerumani kwa kua na magari aina ya Land Rover 613 kwa wakati mmoja hii ikiwa ni kutangaza Utalii na vivutio Jijini hapa kwa kuwa kua na aina ya magari hayo elfu moja (1000) kwa wakati mmoja

Aidha,mwezi june 2024 yalifanyika Maonesho ya Karibu Kili Fair 2024 kwa awamu ya tisa likiwa ni jukwaa maalum la kuyaweka pamoja makampuni ya ndani na nje ya nchi yanayohusika na sekta ya Utalii ambapo wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi waliweza kushiriki.

Vile vile ndani ya Kikao kazi hiki nitaomba kwa ridhaa yako Mhe Rais viongozi hawa waweze kukutana na wa fanya biashara mbalimbali wa mkoa huu ambapo siku hiyo ya tar 29 tutachinja ng'ombe zaidi 200 Iwe ni kula na kunywa ili waweze kufahamiana na viongozi hawa kwani wengine wanawaona kwenye luninga na mitandaoni au kwenye Mikutano na hawapati nafasi ya kuwa karibu nao. Alisema Makonda.

"Mahusiano haya yatatuondolea migogoro mingi, malalamiko mengi na hakika tutawaondoa watu waliowateka wafanyabiashara na kuwafanya kama vitega uchumi vyao kwaajili ya kuwapeleka kwa viongozi.Nakushukuru sana Mhe. Rais kwa kutukubalia ombi letu Taasisi za umma wanaokutana kwenye kituo cha kimataifa cha mikutano AICC Jijini Arusha. Alisema Makonda.

Kwa upande wake Msajili wa hazina Bw. Nehemiah Mchechu amesema Ofisi yake imeandaa na kukamilisha mfumo mpya wa ofisi ambao umezingatia mazingira ya sasa ya kiuchumi, kisheria, kibiashara na kijamii ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Mchechu ameongeza kuwa “tuna vigezo 10 ambavyo tunavitumia naomba nikiri mbele yako katika Taasisi hizi kuna Taasisi 57 ambazo bado zina changamoto ya kufurahia ule uhuru wa kujiendesha, katika hili tumekuwa na mazungumzo na tumekubaliana kama Taasisi tukae pamoja na kuweka mambo yetu sawa’’

“Kwa kuzingatia mapungufu yalibainishwa katika sheria ya sasa ya msajili wa hazina, uchambuzi wa kina ulifanyika na kwenda kutengeneza sheria mpya ya Mamlaka ya uwekezaji wa Umma, tunamatumaini makubwa sana kwamba sheria hii itakamilika katika bunge hili lakini ndani ya mwaka huu’’ amesema Mchechu na kuongeza:

"Katika utekelezaji wa haya mambo Mhe. Rais tumetekeleza maagizo yako ya kuzingatia mapungufu yaliyopo katika Taasisi za kibiashara na za kimkakati na katika hili, tulifanya uchambuzi wa kina kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina, kupitia waraka wetu namba moja wa mwaka 2023 na kuangalia ni Taasisi zipi zipewe uhuru wa kujiendesha’’alisema.











No comments:

Post a Comment