Wednesday 28 August 2024

TBN WANOLEWA NA MTAALAMU WA AKILI BANDIA KUHUSU USALAMA MTANDAONI

 

Wanachama wa Tanzania Bloggers network (TBN) imeshauriwa kuanza kushughukikia kwa ukamilifu  dhima ya uhalisia wa maudhu ya uandishi wa habari kwa kufuatilia na kuthibitisha asili, historia, na umiliki wa maudhui ya kidijitali (Content Provenance) ikiwa ni harua muhimu katika kupambana na Akili Mnembo ama Akili Bandia ama AI.

Imeelezwa kwamba kuna muhimu sana wa kuchukua tahadhari na hatimaye hatua kupambana na swala hilo kutokana na changamoto zinazotokana na teknolojia ya AI, hususan kutokana na kuibuka kwa teknolojia za kizazi kipya kama vile deepfakes. 

“Hapa kuna sababu kwanini uhalisia wa maudhui ni muhimu katika mazingira haya ya kiteknolojia”, mtaalamu wa mambo hayo kutoka Marekani, Bi Amy Larsen, amesema.

Bi Larsen alikuwa anaongea katika mjadala kuhusu mada: "Ushiriki wa Kiraia, Uelewa wa Vyombo vya Habari, Deepfakes, na Kuhusu Maudhui Katika Enzi ya AI, ulioandaliwa na Ubalozi wa Marekani jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa  na waandishi wa maudhui ya Mitandao ya Kijamii Bloggers Network  (TBN) na The CHANZO katika Kituo cha Marekani, Makumbusho ya Taifa, Mtaa wa Shaaban Robert, jijini Dar es Salaam
Bi. Larsen, ambaye ni ni Mkurugenzi wa Mikakati na Usimamizi wa Biashara katika timu ya Democracy Forward ya kampuni ya Microsoft amesema ni lazima kupambana na Taarifa za Kupotosha kwani   kuenea kwa maudhui yanayotokana na AI, kama vile deepfakes, imekuwa rahisi zaidi watu wenye nia mbaya kuunda picha, video, na sauti bandia zinazoweza kupotosha na kudanganya watu.

Mtaalamu huyo ambaye anashika nafasi muhimu katika kusimamia mipango inayohusiana na usalama wa mtandao, taarifa potofu na habari za uongo, uadilifu wa uchaguzi, ulinzi wa uandishi wa habari wa ndani, na kukuza ushiriki wa kiraia wa kampuni, amesema mwaka wa 2024 na 2025 ni miaka muhimu kwa demokrasia na teknolojia, ikizingatiwa kuwa dadi kubwa ya watu kote ulimwenguni watapiga kura kwa ajili ya viongozi wao, huku maendeleo ya haraka ya AI yakileta fursa pamoja na changamoto kubwa kwa wakati mmoja.

Amesema moja ya wasiwasi mkubwa ni matumizi mabaya ya AI kuunda "deepfakes"—video, sauti, na picha bandia halisi ambazo zinaweza kudanganya wapiga kura kwa kubadilisha sura, sauti, au vitendo vya wanasiasa. 

“Hii inasisitiza tofauti kubwa kati ya ahadi ya ubunifu wa kiteknolojia na hatari zake, hasa katika michakato ya kidemokrasia”, amsesisitiza Bi Larsen.
Akiongelea hatua za haraka zinazochukuliwa kupambana na changamoto hiyo, Bi Larsen ameeleza kwamba kampuni 20 za teknolojia zimeungana kuanzisha mpango mpya uitwao Tech Accord to Combat Deceptive Use of AI in 2024 Elections, uliozinduliwa kwenye Mkutano wa Usalama wa mtandao mjini  Munich, Ujerumani, hivi karibuni.

Amesema lengo kuu la makubaliano haya ni kupambana na matumizi ya deepfakes zinazozalishwa na AI ambazo zinaweza kudanganya maoni ya umma na kuhatarisha uadilifu wa chaguzi. 

“Juhudi hii si ya upande wowote wa kisiasa na inaheshimu uhuru wa kujieleza, badala yake inalenga kuhakikisha wapiga kura wanafanya maamuzi sahihi bila kupotoshwa na taarifa za bandia zinazozalishwa na AI”, amesema.

Amesema juhudi hizo zitasaidia waandishi wa habari na mashirika ya vyombo vya habari ambavo hutegemea uaminifu na uadilifu, kuanzisha mnyororo wazi wa uhalisia, vituo vya habari vinaweza kuthibitisha kuwa picha na video wanazochapisha ni halisi na hazijabadilishwa. 

Hii itasaidia kulinda uadilifu wa habari wanazotoa na kuhakikisha kuwa wasikilizaji wao wanaweza kuamini habari wanazopokea. Katika enzi ambayo habari za uongo ni tatizo kubwa, uhalisia wa maudhui unaweza kuwa kinga kwa viwango vya uandishi wa habari.

Bi Larsen ametoia wito kwa Tanzania kuwa macho wakati huu ambapo teknolojia za AI zinaendelea kukua, na umuhimu wa uhalisia wa maudhui ukiendelea kuongezeka. 
Katika hatua nyingine Balozi Larsen alisema ipo haja kubwa kwa Tanzania kushiriki kikamilifu katika mpango huu mpya wa usalama mtandao wa  Tech Accord to Combat Deceptive Use of AI in 2024 Elections, ambao amsesema unatoa mfumo muhimu wa kuthibitisha uhalisia, kulinda dhidi ya taarifa za kupotosha, na kudumisha imani katika mwingiliano wa kidijitali. 

“Kwa kuwekeza katika mifumo imara ya uhalisia, tunaweza kuhakikisha kuwa faida za AI zinatimizwa huku tukipunguza hatari zinazohusiana na matumizi mabaya ya teknolojia hii”, alisema Larsen.

No comments:

Post a Comment