Monday, 13 June 2016

WAJASIRIAMALI KUTOKA TASWE WAULA MKATABA WA BIASHARA NCHINI COMORO

 

 Picha ya pamoja ya wawakilishi wa wajasiriamali wanawake wa Tanzania Saccoss Women Enterpreneurs (TASWE) waliopata fursa ya kushiriki maonesho ya biashara nchini Comoro
 
Baadhi ya wajasiriamali kutoka Tanzania wakiwa uwanja wa Mwl. Julius Kambarage Nyerere tayari kwa safari ya kwenda nhini Comoro


Ziara ya Kikundi cha Wajasiriamali Wanawake kutoka Tanzania (Tanzania Saccos for Women Enterpreneurs) TASWE imezaa matunda baada ya kikundi hicho cha kina mama kufanikiwa kuingia mkataba wa ushirikiano (MoU) katika masuala ya biashara na Kikundi cha Wanawake Wajasiriamali wa Comoro (Association of Women Entrepreneurs in Comoro).


Makubaliano hayo ya ushirikiano yalifikiwa kufuatia ziara ya siku mbili iliyofanywa na Kikundi cha Wajasiriamali Wanawake kutoka Tanzania nchini Comoro walifanikiwa kuondoka tarehe 13 Juni 2016 na kurudi . Lengo la ziara hiyo ilikuwa kutafuta masoko kwa ajili ya bidhaa za Tanzania nchini Comoro, pamoja na kukutana na wajasiriamali wa Comoro ili kuweza kubadilishana taarifa juu ya fursa mbalimbali za biashara kati ya Tanzania na Comoro.

Tukio hilo la utiaji saini wa makubaliano ya ushirikiano baina ya vikundi hivyo vya Wajasiriamali akina mama kutoka Tanzania na Komoro lilishuhudiwa na Balozi wa Tanzania nchini Komoro Mhe. Chabaka F. Kilumanga. Katika hafla hiyo, Mhe. Balozi Kilumanga aliwapongeza wajasiriamali hao kwa hatua hiyo muhimu waliofikia na kuwa ana imani ushirikiano huo utakuwa ni wakudumu na wenye manufaa kwa pande zote mbili. Alieleza kuwa Tanzania na Comoro zinaweza kushirikiana katika nyanja mbalimbali za biashara na ana imani kuwa hii itakuwa ni chachu kwa wawekezaji wengine kutoka Tanzania kuja nchini Comoro kwa ajili ya kuekeza.
Bi. Naila Thabeet wa Association of Women Enterpreneurs akibadilishana mkataba na Bi Anna Matinde Mwenyekiti kutoka Tanzania Saccoss for Women Enterprenuers (TASWE)
Wadau wakishuhudia tukio la kihistoria ambapo ni mara ya kwanza vikundi vya akina mama kutoka Komoro na Tanzania wamekubaliana kushirikiana katika nyanja za biashara.

Baadhi ya bidhaa walizoweza kwenda kuziuza comoro ni kama picha zifuatazo zinavyoonyesha






No comments:

Post a Comment