Monday, 31 August 2015

CCM Yaja na Sera ya Elimu Bure Hadi Form IV

Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu amesema chama hicho kikichaguliwa na Watanzania kuunda Serikali tena kitahakikisha kinaweka utaratibu mzuri utakaomfanya mwananchi mfanyabiashara kupenda kulipa kodi kwa ajili ya maendeleo. Samia ametoa ahadi hiyo Mjini Mbulu alipokuwa akiwahutubia wananchi na wanaCCM katika mkutano wa hadhara wa kampeni za chama hicho. Alisema watahakikisha wanaondoa kodi za hovyo hovyo ambazo zimekuwa zikitozwa hivi sasa katika maeneo anuai. "...Tutaweka utaratibu mzuri ambao utamfanya mwananchi apende kulipa kodi, ila kodi za hovyo hovyo tutaziondoa...," alisema mgombea huyo mwenza wa urais akiilani ilani ya CCM na kumuombea kura mgombea urais wa chama hicho, Dk. John Pombe Magufuli. Akihutubia mkutano mwingine Jimbo la Babati Mjini Bi. Suluhu alisema serikali itakayoundwa na Chama Cha Mapinduzi ili kuboresha sekta ya elimu itahakikisha inatoa elimu bure kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne jambo ambalo pia litawapunguzia mzigo familia na kutoa fursa sawa ya elimu ngazi ya msingi na sekondari (kidato cha nne). Aidha alisema serikali itakayoundwa na CCM pia itahakikisha inafanya maboresho makubwa katika sekta ya afya, umeme, huduma za maji safi na salama pamoja na kuwawezesha wananchi hasa makundi ya vijana na akinamama. Alisema katika maeneo ya wafugaji watahakikisha wanashirikiana na halmashauri kupima na kuweka mipaka ya ardhi katika vijiji ili kuondoa mvutano wa wakulima na wafugaji. Kuwasaidia wafugaji kujenga majosho ya nifugo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa viwanda vya kuchakata bidhaa za mifugo kuziongezea thamani. Hata hivyo aliwahakikishia wanavijiji ambao wamekumbwa na ukame kuwa Serikali imejipanga kuwasaidia hivyo hakuna mwanakijiji atakaye kufa kwa njaa. Pamoja na hayo alisema Serikali ijayo ya CCM ili kuongeza kasi ya uwajibikaji imepanga kuunda kitengo maalumu cha kupokea na kushughulikia kero na malalamikoa ya wananchi, jambo ambalo litaweka bayana nani hataki kuwajibika kazini.
Mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu (hayupo pichani) akinadi ilani ya Chama Cha Mapinduzi Jimbo la Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba. Mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu (hayupo pichani) akinadi ilani ya Chama Cha Mapinduzi Jimbo la Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba. 

Baadhi ya wanaCCM na wananchi wakimsikiliza mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Babati Mjini. Baadhi ya wanaCCM na wananchi wakimsikiliza mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Babati Mjini

Mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu kushoto akihutubia wanaCCM na wananchi babati Mjini. Mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu kushoto akihutubia wanaCCM na wananchi babati Mjini.

Mbunge anaemaliza muda wake jimbo la Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba kabla ya mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu kupanda jukwaani kunadi sera za CCM. Mbunge anaemaliza muda wake jimbo la Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba kabla ya mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu kupanda jukwaani kunadi sera za CCM.

Mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu akiwa jukwaani akinadi ilani ya Chama Cha Mapinduzi Jimbo la Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba. Mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu akiwa jukwaani akinadi ilani ya Chama Cha Mapinduzi Jimbo la Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba.

No comments:

Post a Comment