Tuesday, 1 September 2015

PSPF YAZINDUA HUDUMA YA KUKOPESHA VIWANJA KWA WANACHAMA WAKE

 
Mfuko wa Pensheni wa PSPF kwa kushirikiana na Benk ya Posta Tanzania (TPB) na Taasisi ya Property International Ltd (PIL) wamezindua mpango maalum wa kutoa mikopo ya viwanja kwa wanachama wa mfuko huo.
 
Picha ya pamoja na wafanyakazi wa PSPF

Lengo la mkopo huu wa viwanja ni kuwawezesha wanachama wa mfuko huu kumiliki viwanja vilivyopimwa na vilivyo halali kwa mujibu wa taratibu za nchi. Nia ni kwenda sambamba na dira ya PSPF ambayo ni kutoa huduma bora zenye ushindani katika sekta ya Hifadhi ya Jamii kwa wateja wa PSPF, na pia kuitikia mwito wa Mamlaka ya Uhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), walioagiza Mifuko yote ya Hifadhi ya Jamii kutoa mafao kwa fomula iliyo sawa kwa watumishi wote. Hivyo kuanzia wakati huo Mifuko ya Hifadhi inapaswa kushindana kwa ubora wa huduma na vivutio vingine kwa wanachama na wanachama watarajiwa.
Ni dhahiri kuwa kila Mtanzania anahitaji kuwa na makazi bora ya kudumu, hivyo mpango huu uliozinduliwa ni mpango mzuri sana hasa kwa Watanzania wengi ambao hawana uwezo wa kutoa fedha taslimu. Utaratibu huu wa kuwakopesha wanachama utawanufaisha wengi na hatimaye kufikia kauli mbiu ya serikali yetu ya kuhakikisha Maisha bora kwa kila Mtanzania.
Mfuko wa Pensheni wa PSPF umeendeleza ushirikiano wake mzuri na Benki ya Posta Tanzania, ambapo kama mnavyofahamu ushirikiano wao ulianzia kwenye utoaji wa Mikopo kwa Wastaafu, Mkopo wa Elimu na Mkopo wa kuanzisha Maisha kwa wanachama wapya. Jitihada  hizi zote ni katika kuhakikisha PSPF inatoa huduma bora kwa wanachama wake, na pia katika kuonyesha imani kwa benki ya Posta, ambayo huduma zake bora zinapatikana kote nchini. Mahusiano haya na Property International Ltd yanazidi kujenga mahusiano haya kwa maslahi ya wanachama na Watanzania kwa ujumla.
Wanachama wa PSPF waliochangia mfuko kwa kipindi kisichopungua miezi sita wanasifa zote za kuweza kukopa viwanja hivi, na watapaswa kulipa ndani ya miaka mitatu. Wanachama walio katika mpango wa Uchangiaji wa Hiari pia watafaidika na mkopo huu. 

 

 Picha ya pamoja na wafanyakazi wa Property International Ltd (PIL)


 Mkurugenzi wa uwekezaji wa mfuko wa PSPF Ndugu Gabriel Silayo akifafanua kwa ufasaha mpango mzima wa huduma ya kukopesha Viwanja kwa Wanachama wa PSPF.

 

 Afisa Mtendaji Mkuu wa bank ya Posta TPB Sabasaba  Moshingi akitoa hotuba



Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Raisi Mh. Samia Suluhu Hassan naye alipata wasaa wa kuongea

 
Afisa Mtendaji wa PIL akielezea jinsi mpango mzima utakavyo endeshwa na kufanikiwa.




   Mrisho Mpoto na kikosi chake wakitoa burudani



Picha ya Pamoja na Wafanyakazi wa Tanzania Posta Bank TPB


Picha ya pamoja na Mpoto akiwa na team yake ya Mjomba Group

Wanachama wote wa Mfuko wa Hifadhi wa PSPF wanakaribishwa sana kupata mkopo huu maalum kwa ajili yao.

No comments:

Post a Comment