Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu amesema
chama hicho kikichaguliwa na Watanzania kuunda Serikali tena
kitahakikisha kinaweka utaratibu mzuri utakaomfanya mwananchi
mfanyabiashara kupenda kulipa kodi kwa ajili ya maendeleo. Samia ametoa
ahadi hiyo Mjini Mbulu alipokuwa akiwahutubia wananchi na wanaCCM katika
mkutano wa hadhara wa kampeni za chama hicho.
Alisema watahakikisha wanaondoa kodi za hovyo hovyo ambazo zimekuwa
zikitozwa hivi sasa katika maeneo anuai. "...Tutaweka utaratibu mzuri
ambao utamfanya mwananchi apende kulipa kodi, ila kodi za hovyo hovyo
tutaziondoa...," alisema mgombea huyo mwenza wa urais akiilani ilani ya
CCM na kumuombea kura mgombea urais wa chama hicho, Dk. John Pombe
Magufuli.
Akihutubia mkutano mwingine Jimbo la Babati Mjini Bi. Suluhu alisema
serikali itakayoundwa na Chama Cha Mapinduzi ili kuboresha sekta ya
elimu itahakikisha inatoa elimu bure kuanzia darasa la kwanza hadi
kidato cha nne jambo ambalo pia litawapunguzia mzigo familia na kutoa
fursa sawa ya elimu ngazi ya msingi na sekondari (kidato cha nne).
Aidha alisema serikali itakayoundwa na CCM pia itahakikisha inafanya
maboresho makubwa katika sekta ya afya, umeme, huduma za maji safi na
salama pamoja na kuwawezesha wananchi hasa makundi ya vijana na
akinamama. Alisema katika maeneo ya wafugaji watahakikisha
wanashirikiana na halmashauri kupima na kuweka mipaka ya ardhi katika
vijiji ili kuondoa mvutano wa wakulima na wafugaji.
Kuwasaidia wafugaji kujenga majosho ya nifugo ikiwa ni pamoja na ujenzi
wa viwanda vya kuchakata bidhaa za mifugo kuziongezea thamani. Hata
hivyo aliwahakikishia wanavijiji ambao wamekumbwa na ukame kuwa Serikali
imejipanga kuwasaidia hivyo hakuna mwanakijiji atakaye kufa kwa njaa.
Pamoja na hayo alisema Serikali ijayo ya CCM ili kuongeza kasi ya
uwajibikaji imepanga kuunda kitengo maalumu cha kupokea na kushughulikia
kero na malalamikoa ya wananchi, jambo ambalo litaweka bayana nani
hataki kuwajibika kazini.
Mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu (hayupo pichani) akinadi ilani ya Chama Cha Mapinduzi Jimbo la Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba. Baadhi ya wanaCCM na wananchi wakimsikiliza mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Babati Mjini
Mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu kushoto akihutubia wanaCCM na wananchi babati Mjini.
Mbunge anaemaliza muda wake jimbo la Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba kabla ya mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu kupanda jukwaani kunadi sera za CCM.
Mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu akiwa jukwaani akinadi ilani ya Chama Cha Mapinduzi Jimbo la Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba.
0 comentários :
Post a Comment