TCRA KUWANOA TANZANIA BLOGGERS NETWORKING (TBN) KULINDA TAARIFA BINAFSI UCHAGUZI 2025

BLOGA WANAJUKUMU LA KUELIMISHA JAMII SHERIA YA ULINZI WA TAARIFA BINAFSI

PDPC Innocent Mungy akiwafua wana Blogu Tanzania


Waandishi wa habari na mabloga wametakiwa kuelimisha jamii kuhusu sheria ya ulinzi wa taarifa binafsi, ili kuzuia uvunjifu wa faragha na kuepusha madhara ya kisheria.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Uhusiano na Mawasiliano kwa Umma wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC), Innocent Mungy, wakati wa mafunzo maalum kuelekea Uchaguzi Mkuu, yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa ombi la Mtandao wa Mabloga Tanzania (TBN).

Mungy alisema mabloga wana nafasi kubwa ya kuelimisha umma kuhusu sheria hiyo, hasa katika kipindi cha uchaguzi, na kuwaonya kuepuka kuchapisha taarifa binafsi za watu au wagombea.
PDPC imesisitiza Mabloga Kulinda Taarifa Binafsi Uchaguzi 2025

Meneja wa Huduma za Utangazaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mhandisi Andrew Kisaka, akiwasilisha mada katika mafunzo maalumu kuelekea uchaguzi mkuu mahususi kwa bloga yaliyoandaliwa na  Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Agosti 11, 2025 Jijini Dar es Salaam.

Pichani ni mabloga mbali mbali nchini wakiwemo Habarika Blogu, Michuzi Blogu, Kajunason Blogu, Lukwangule Blogu, Bongoweekend Blogu na zingine nyingi



Mwenyekiti wa TBN, Beda Msimbe, aliishukuru Serikali chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fursa ya mafunzo hayo kupitia TCRA, akisema yatasaidia kuongeza weledi na kuimarisha usalama wa taarifa wakati wa uchaguzi




About Judith Mwaheleja

I am a Tanzanian Blogger , Entrepereneur and Fashonista.

0 comentários :

Post a Comment