Wednesday, 28 August 2024

YANGA WATIA TIMU BUKOBA KUZISAKA ALAMA TATU.

Na Dulla Uwezo


Kikosi cha Timu ya Yanga Africans Kimewasili salama Bukoba Mjini Tayari kuzitafuta alama Tatu Muhimu, katika Mchezo wao utakaopigwa Tarehe 29 Agosti katika Dimba la Kaitaba dhidi ya Wenyeji wao Kagera Sugar Wanankurukumbi.

Kikosi Kimewasili majira ya Saa Sita Mchana na Ndege, Kisha Kuelekea mapumZiko mafupi Hotelini kabla ya Kufanya Mazoezi jioni ya Leo Tayari kukabiliana na Wakata Miwa wa Kagera.

Mapema Asubuhi ya jana Baadhi ya Wapenzi na Mashabiki wa Timu ya Yanga Mkoani Kagera hususani Wakazi wa Bukoba wameungana katika Tukio la Kula na Kunywa Supu maarufu kama Supu Day lililoratibiwa na Uongozi wa Yanga Tawi la Bukoba Mjini, chini ya Mratibu Jamali Kalumuna (Jamco) Tukio lilikambatana na Usajili wa Wananchama wapya huku Wanachama wengine wakikumbushwa juu ya ulipaji wa Ada










No comments:

Post a Comment