Wednesday, 13 September 2017

TACAIDS WAFANIKIWA KUTHIBITI UKIMWI


MAAMBUKI ZI ya Virusi vya ukimwi nchini yameteremka kutoka asilimia 5.7 kwaka 2007 na  mwaka 2008 hadi kufikia asilimia 5.1 mwaka 2011 na 2012.

Hayo yamebainishwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji  wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Jumanne Issango wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, kuhusu majukumu ya tume hiyo, mafanikio, changamoto na muelekeo wa baadaye.

 Alisema kiwango cha maambukizi ya virusi vya ukimwi kinaendelea kupungua kutoka aslimia 0.32 kwa kipindi cha mwaka 2012 na kitafikia hadi asilimia 0.16 ifikapo mwaka 2018.

Issango alisema kuongezeka kwa idadi ya watu wanaopata huduma na tiba ya VVU ikiwa ni mapoja na dawa za kupunguza makali ya ukimwi kutoka watu 333,517 mwaka 2010 hadi kufikia 650,003 mwaka 2015 na kuanzisha na kuimarisha ofisi za waratibu wa ukimwi wa mikoa TACAIDS kwenye mikoa yote ya Tanzania Bara.

Aliongeza kuwa mpango mwingine ni kuwezesha mikoa 21 na Halmshauri 133 kuweka mifumo ya kuweza kutumia Tehama kwa utoaji taarifa na upashanaji wa habari na kuhifadhi data ya Tomsha.

Alisema tayari mfuko wa udhamini wa shughuli za kudhibiti ukimwi (ATF) 2015 umeanzishwa  na serikali imeanza kuchangia sh.bilioni 3 kwa mwaka wa fedha wa 2015 na 2016.

Akizungumzia changamoto zilizopo Issango alisema ni upungufu wa rasilimali fedha za mapambano dhidi ya ukimwi kwa kuwepo kwa vyanzo vilivyo endelevu, unyanyapaa katika jamii pamoja na uelewa mkubwa wa wananchi kuhusu ukimwi na kubadili tabia hakuendani na kiwango cha elimu ya ukimwi.

Alisema muelekeo na matarajio ni kutekeleza kwa ufanisi mfuko wa kudhibiti ukimwi ambapo serikali imeanzisha mfuko huo ndani ya tume ambapo utaweza kupanua wigo wa ukusanyaji rasilimali fedha ndani ya nchi na kuongeza ushiriki wa sekta isiyo ya serikali katika mapambano dhidi ya ukimwi.
.

Kaimu Mkurugenzi Idara ya mwitikio wa kitaifa, Audrey Njelekela,   ameitaja mikoa inayoongoza kuwa na maambukizi ya virusi vya ukimwi kuwa ni pamoja na Njombe na Iringa ambapo mikoa iliyo chini kwa maambukizi ni Manyara ,Tanga na Lindi.

Aidha ameeleza kuwa TACAIDS inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na unyanyapaa wanaokutana nao waathirika wa ugonjwa wa ukimwi, upungufu wa raslimali-fedha baada ya wafadhili kuondoka na kuongezeka kwa watoto yatima.
  Kaimu Mkurugrnzi Mtendaji  wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Jumanne Issango akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, wakati akitoa taarifa  kuhusu majukumu ya tume hiyo, mafanikio, changamoto na muelekeo wa baadaye. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa  Tume hiyo , Nadhifa Omar

 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa  Tume hiyo , Nadhifa Omar. , Nadhifa Omar akizungumza wakati akimkaribisha Kaimu Mkurugenzi kuzungumza na wanahabari.
 Waandishi wa habari wakichukua taarifa hiyo.

 Mkutano na wanahabari ukiendelea.

 Kaimu Mkurugenzi wa Muitikio wa Kitaifa wa VVU, Audrey Njelekela, akizungumza katika mkutano huo.

Mkurugenzi wa Sera, Utafiti na Mipango wa tume hiyo, Richard Ngirwa akizungumza kwenye mkutano huo.



No comments:

Post a Comment