Sunday, 4 August 2024

PSSSF KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI YAWAALIKA WANACHAMA NANENANE 2024 VIWANJA VYA JOHN MWAKANGALE


NA MWANDISHI WETU, DODOMA

Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) unawaalika wananchama na wananchi kutembelea banda la Mfuko huo katika Maonesho ya Wakulima, Wafugaji na Wavuvi (Nane Nane) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini yanayofanyika katika iwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.

Kanda ya Nyanda za Juu Kusini inajumuisha Mikoa ya Iringa, Njombe, Songea, Mbeya, Songwe, Rukwa na Katavi.

Akizungumzia ushiriki wa PSSSF kwenye Maonesho hayo, Kiongozi wa banda PSSSF, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Bw. Edward Kyando, amesema, Mfuko huo unawahudumia Watumishi wa Umma, ambao nao ni washiriki katika Maonesho hayo wakiwakilisha taasisi zao.

“Lakini si tu watumishi ambao ni wanachama wetu, pia kuna fursa mbalimbali za kiuchumi kupitia uwekezaji wa Mfuko kwenye maeneo ya viwanda, lakini pia majengo na nyumba za makazi, hivyo wananchi nao wanakaribishwa kupata taarifa za fursa zinazopatikana PSSSF.” Amesema.

Kwa wananchama watakaotembelea banda la PSSSF watapata taarifa mbalimbali zinazohusiana na uanachama wao kama vile, Taarifa za Michango, Taarifa za Mafao, Taarifa za Uwekezaji na pia wanachama wataelimishwa jinsi ya kupata huduma kupitia mtandao maarufu PSSSF Kidijitali.

“Huduma hii ya PSSSF Kidijitali, inamuwezesha Mwanachama kujihudumia mwenyewe kupitia simu janja kupitia, atapata huduma zote ikiwa ni pamoja na kuwasilisha madai mbalimbali. Halikadhalika kwa wastaafu nao wanaweza kujihakiki.” Alifafanua.

Kauli Mbiu ya Maonesho ya mwaka huu ni “Chagua Viongozi Bora wa Serikali za Mitaa kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi”.


Afisa wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw. Emilyo Mwakalobo (kushoto), akimuhudumia mwanachama wa Mfuko huo aliyetembelea Maonesho ya Wakulima, Wafugaji na Wavuvi (Nane Nane) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini yanayofanyika katika iwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.

Afisa wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw. Edward Nzota (kushoto), akimuelekeza mwanachama wa Mfuko huo jinsi ya kutumia PSSSF Kidijitali kupitia simu yake mkononi (simu janja) kwenye banda la PSSSF kwenye Maonesho ya Wakulima, Wafugaji na Wavuvi (Nane Nane) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini yanayofanyika katika iwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.
Edward Nzota (kulia) Mfanyakazi wa PSSSF, akifurahia jambo na Mwanachama wa Mfuko huo aliyefika kuhudumiwa

Timu ya Maafisa wa PSSSF ikiwa tayari kuwahudumia wanachama na wananchi katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya. Kutoka kushoto kwenda kulia ni Edward Nzota, Emilyo Mwakalobo, Swinford Mndellah, Joyce Mtinangi na Edward Kyando.
Mwanachama, akizungumza mbele ya wafanyakazi wa PSSSF alipotembelea banda la Mfuko huo kuhudumiwa
Timu ya PSSSF Nanenane 2024 Kanda ya Njanda za Juu Kusini, viwanja vya John Mwakangale, jijini Mbeya.

No comments:

Post a Comment