Wednesday, 4 April 2018

PINGA UKATILI WA WANAWAKE TANZANIA

Mpaka karne hii bado mila potofu zinaendelea kutumika katika jamii, mila ambazo zinaendelea kuwanyanyasa kijinsia wanawake na kuwafanya wajione sio kitu katika jamii.


Mapema mwezi April nilipata fursa ya kuambatana na shirika la kivulini mjini Tarime tukiwa chini ya ufadhili wa Oxfam Tanzania na kuzungukia mikoa ya Mara hii ni pamoja na Shinyanga, Mwanza, Musoma Tarime na Butihama.
Huko tulikutana na changamoto nyingi wanazopitia wakina mama na watoto bila ya kuwa na msaada wowote katika jamii au serikalini.


Picha ya Judy Mwaheleja
Mzee wa mila Tarime pichani ambaye mwenye nyazifa ya uwenyekiti wa mila akithibitisha ukeketaji kwa mabinti wadogo unaendelea kijijini hapo ili kudumisha mila mwanamke akiolewa atulie na mume mmoja.


Wazee wa kijiji ambao ndio wana madaraka ya shughuli za kimila na ambao wanaheshimiwa hawajaweza kuwa msaada kwa wamama hawa na mabinti kwani bado sehemu kubwa ya tarime wanaendeleza mila hizo potofu kwa manufaa yao binafsi ya kujipatia kipato. Walituhoji wakiacha hiyo mila watakula wapi?


Tumegundua ukeketaji wa mabinti wadogo umekithiri na kupelekea watoto kufariki katika zoezi hilo kwani hawatumii njia sahihi za kuwakata maumbile yao na kuwapelekea kupoteza damu nyingi sana wakati mwingine inawapelekea kupata Vistula hapo baadae.
Kipindi cha ukeketaji watoto wa kike wanachukuliwa na kupelekwa maporini hii inawapotezea vipindi vya masomo yao na kushindwa kufanya mitihani yao vizuri
Kwakweli tumeona kabisa hamna msaada kwa mabinti hawa kwasababu mama zao hawana sauti katika familia na hata wakienda kushitaki polisi wanaambiwa ni mgogoro wakifamilia warudi waelewane kifamilia na hata wakiwakimbilia wazee wa kijiji huko ndiko wanakamatwa kabisaa na kufanyiwa vitendo hivyo kwani hawa wazee wa mila ndio biashara yao na wanajipatia riziki kwa kupitia shughuli hii. Kwa binti mmoja akikeketwa wanalipwa sh 25 elfu tunaona hapo ina sababisha kuwa vigumu kuangamiza vitendo hivyo vya kiukatili.
Makabila mengi ya Mara mwanamke kupigwa adharani hadi kuvuliwa nguo hiyo ndio sifa ya baba kuwa na yeye ni mume
Uzalilishaji wa kukeketwa mabinti umekithiri yote hayo wakiamini wanadumisha mila ili wazazi waweze kupata ng'ombe wengi maana mabinti watatulia hadi siku watakapo olewa, kwao lengo kwa mtoto wa kike si elimu au aje kuwa kiongozi Fulani au daktari wenyewe wanawaza atafikisha lini miaka 15 ili aweze kuolewa na kipindi hicho cha kuolewa kwakwe ng'ombe wangapi atapata.
Unyanyasaji unaendelea mpaka kwa mama mtoto maana baba anachukua mtaji wa ng'ombe wa mtoto wa kike aliyemuozesha na yeye anaenda kuongeza kuoa mke wapili ambapo analeta uadui kati ya wake zake. Hakuna atakaye furahia mahali ya mwanae halafu unaenda kuniolea mke mwingine! kwakweli hali inasikitisha.


Picha ya Judy Mwaheleja
Nikiwapa elimu mabinti watambue haki zao za msingi ikumbukwe kuwa Ukatili Sio Jibu project hii ilikuwa chini ya uzamini wa Oxfam Tanzania.


Tuliweza kuwaita wazee wa mila na kuwapa elimu ya umuhimu wa haki za wanawake akiwemo Mwenyekiti wa mila, Askari polisi dawati la jinsia, Diwani wa halmashauri ya Tarime na wananchi mbali mbali waliokumbwa na janga na wengine walio shuhudia vitendo hivyo vya kikatili. Lakini tukagundua sisi pekee haitatosha kukabiliana na matatizo wanayokumbana nayo wanawake na mabinti wa mikoa ya Mara.
Picha ya Judy Mwaheleja


Basi nini kifanyike ili kutokomeza hali hiyo?
Kwanza wazee wa mila waangaliwe na wawezeshwe kiuchumi ili nazani litafanyiwa kazi na diwani wa maeneo husika wataweza kuwasilisha taarifa kwenye ngazi za juu. Kwakufanya hivyo tutaweza kuwafanya wazee wa mila na wananchi wa maeneo kuwa na kauli moja ya HAPANA ukeketaji na udhalilishaji wa mwanamke. Kila mmoja atamlinda mwanamke.
Uthubutu kwa wahanga wa unyanyasaji kuweza kupaza sauti watakapo ona wanataka kutendewa vitendo vya ajabu. mfano kama mama anajua kuna mipango ya baba kumpeleka mtoto wa kike kukeketwa basi awajulishe jamii inayowazunguka kwapamoja waje wazuie.
Sheria nyingine zifanyiwe marekebisho ushahidi wa mahakamani uangaliwe upya mtu akishitaki amebakwa na mtu fulani basi ripoti ya daktari ikidhibitisha mshatakiwa apewe athabu kali na sio unamwambia mtu leta shahidi sasa shahidi atamtoa wapi wakati vipimovina sema kafanyiwa ukatili fulani na anakuambia ni huyu. Watuhumiwa wasipochukuliwa hatua wanarudi kulipa kisasi na kuwafanya wengine waogope kupaza sauti.







No comments:

Post a Comment