Wednesday, 7 December 2016

NMB YAFUNGULIA NJIA TBN SERIKALI WA AHIDI KUANDAA TUZO ZA BLOGGER NCHINI

Mkutano wa chama cha ma bloggers Tanzania wafana kwa siku mbili mfululizo katika ukumbi wa PSPF uliopo Golden Jubilee Tower.
Mkutano huo na mafunzo kwa wanachama yaliwezakuleta tija kwa wanachama waliohudhuria huku kwa pamoja wakiwa na kauli mbiu ya "Mitandao ya kijamii ni Ajira itumike kwa manufaa"
Mkutano uliweza kufunguliwa rasmi na Mkurugenzi wa idara ya habari maelezo na msemaji wa serikali Dk. Hassan Abasi, ambapo aliweza kutatua changamoto zinazokabiliwa na waandishi wa mitandao ikiwa ni pamoja na kuahidi kufanyia kazi na kutoa ugumu na vikwazo vyote vinavyokwamisha shughuli za utangazaji mitandaoni. hakuishia hapo bali aliwahakikishia bloggers wote kuwa shughulizao zinatambulika kiserikali na ushirikiano wa bega kwa bega baina ya waandishi hao na serikali.
  
Dk. Hassan Abbasi akijibu hoja za wanachama wa TBN na kutatuachangamoto wanazokutana nazo.


Katibu wa chama cha bloggers Khadija, Mwenyekiti Joakim Mushi, Dk Hassan Abasi pamoja na msemaji wa NMB


Blogger Maxence Melo wa Jamii Forum akitoa mafunzo 

 
Blogger Krants Mwantepele akitoa mafunzo kwa wanachama






Bloggers wakisikiliza kwa umakini

Mbali na mafunzo wanachama wa TBN waliweza kufaidika na mkutano huo kwakufungua account na NMB pia walijiunga na mfuko wa PSPF na kukabidhiwa card zao na mheshimiwa Nape Nnauye ambaye aliudhuria mkutano huo nakutoa fursa mbalimbali kwa chama hicho na mwisho kuhitimisha mafunzo na mkutano huo.
 
Blogger Seria kutoka Arusha akikabidhiwa carNMB pamoja na card ya PSPF


Mh. Waziri Nape Nnauye akizungumza na wanachama wa Tanzania Bloggers Networking

Katika mazungumzo na wanachama wa TBN Mh. Nape aliweza kuwaambia kuwa serikali inawapongeza wana habari hao na watawaungamkono na mwisho kutoa Tuzo kwa blogger atakaye fanya vizuri zaidi.


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgA46AC1jg1gUsdMeJpVVtuVbaV7ju3eSEemIFmB4XVTtire-QGi4x_3hmJQ6-cv50JtTZjIszsGWppB7yNxeanYThczsqBHLs4h0FcvUa3HlOx7wG_S3S0562w5nZ6hFp8TQswAypb95Y/s1600/5R5A6168.jpg
Waziri wa habari, utamaduni sanaa na michezo Mh. Nape Nnauye aliweza kupata fursa ya kuwa mwanachama wa PSPF na kukabithiwa card ya uanachama siku hiyo hiyo.

 
Wanachama wa TBN Issa Michuzi, Seria Tumainiel na Maxence Melo waliweza kuudhuria mkutano mkuu na mafunzo 
 
 Jeedygirl wa Life Goes On Blog

 
Picha ya Pamoja

No comments:

Post a Comment