Wednesday, 2 March 2016

WADAU WAAANZA KUJENGA UELEWA KUHUSU SIKU YA MAGONJWA YANAYOTOKEA KWA KUNDI DOGO LA JAMII

RARE DISEASE DAY 2016 ilifanyika mwishoni mwa mwezi February katika ukumbi wa Ruvu Serena Hotel. Kusudi ilikuwa ni kupaza sauti na watu wagundue kuwa kuna magonjwa yanayotokea kwa kundi dogo la jamii na hatupaswi kuwatenga wanaokumbana nayo.
Wadau hao wakinyoosha mikono juu kuonesha umuhimu wa kuadhimishwa kwa siku hiyo ya Magonjwa Yanayotokea kwa kundi dogo la jamii ndani ya jamii.
Mratibu wa tukio hilo Bibi Sharifa Mbaraka akizungumza mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani) kwenye moja ya ukumbi wa hoteli ya Serena leo jijini Dar,Bi.Sharifa alisema kuwa tukio hilo limedhamiria kujumuisha  vyombo vya habari na wadau wengine ili kujenga uelewa kuhusu magonjwa hayo. 

“Yapo magonjwa tofauti yanayowasibu watu wachache takribani 7000 ambayo yameshabainishwa duniani hadi leo na Tanzania haiwezi kujitoa kwenye  hili. Hata hivyo watu wengi hapa Tanzania hawana uelewa  kuhusu magonjwa hayo”,alisema Bi Sharifa ambaye watoto wake wawili Ali Mohammed Kimara 5, na Nasreem Mohammed 3, wanasumbuliwa na magonjwa hayo.

Alifafanua kuwa kutokana na uzoefu wake, amepata msukumo  na kuamua kuwaunganisha wazazi, wagonjwa walio na magonjwa hayo na raia wenye mapenzi mema ili kujenga uelewa muhimu na kutoa wito kwa jamii kuchukua hatua.

Pichani wa pili kulia ni Mdau mkubwa wa sekta ya afya Monica Joseph kutoka Philips Medical Systems , akifafanua zaidi kuhusiana na huadhimishwa kwa Siku ya 'Rare Disease' Duniani ambayo inaadhimishwa leo.Monica amesema kuwa ni wakati mwafaka kwa Watanzania kuwa na tahadhari ya kuelewa kuhusu magonjwa hayo ili wanajamii waweze kufahamu mbinu za kuyadhibiti iwapo watayakuta ndani ya jamii. pichani kulia ni Dkt.Mariam Nooram kutoka hospital ya Aghakhan.
 
Kauli mbiu ya Siku ya Magonjwa Yanayotokea kwa kundi dogo la jamii Mwaka 2016 ni ‘Sauti za Wagonjwa’ na inamaanisha kutambua mchango muhimu unatolewa na wagonjwa katika kutaka mahitaji yao na kuchochea mabadiliko ambayo yataboresha maisha yao na masiha ya familia zao na maisha ya wale wanaowahudumia. 

Kauli mbiu ya Siku ya Magonjwa yanayotokea kwa kundi dogo la wanajamii ambayo ni, “Ungana nasi kuzifanya sauti za waathirika zisikike” ikitaka jamii kwa jumla, wale wanaishi bila magonjwa hayo au wanaothirika nayo moja kwa moja kuungana na jamii ya waathirika katika kuelewa athari za magonjwa hayo. Watu wanaoishi na magonjwa hayo na familia zao mara kadhaa hutengwa. Jamii inaweza kuwaunganisha kutoka kwenye kutengwa huko. 

Lengo la jumla la Siku ya Magonjwa yanayotokea kwa kundi dogo la jamii ni kuhamasisha uelewa miongoni wa umma kwa jumla kuhusu magonwa hayo na athari zake kwa maisha ya wagonjwa ili kuyapa kipaumbele kwenye afya ya jamii ya Tanzania na kwenye bajeti ya serikali kupitia Wizara husika.

Professor Kareem Manji kutoka Muhimbili akitoa ufafanuzi mbele ya Waandishi wa Habari namna magonjwa hayo yanavyoisumbua jamii kwa kiasi kikubwa na pia uzoefu wake katika suala zima la kutoa matibabu,kushoto kwake ni Dkt Nurudin Lakhan ambaye pia alielezea namna ya magonjwa hayo  Yanayotokea kwa kundi dogo la jamii yanapaswa kuangaliwa upya ili kuitaka jamii kutambua kuwa magonjwa hayo yapo na yamekuwa yakiisumbua jamii kwa muda mrefu.

Bi.Monica Joseph kutoka Philips Medical Systems  alieleza mambo kadhaaa katika kupambana na magonjwa hayo,ameeleza kuwa ipo haja ya wadau wa sekta ya Afya na jamii kwa ujumla kuyafahamu magonjwa yasiyotambulika yapo katika jamii yetu na lazima tuchukue hatua za kushughulika nayo. Miongoni mwa hatua zinazopaswa kuchukuliwa ni pamoja na:
 
( a) Zifanyike juhudi za makusudi kuwapatia wataalam wa afya mafunzo maalum ya kutambua na kutibia magonjwa hayo,( b) Kuanzisha vitengo maalum vya kushughulikia magonjwa hayo hususan kwenye Hospitali za Rufaa. Vitengo hivyo havinabudi kuwa na vifaa mbalimbali vya kusaidia matibabu ya ugonjwa huo,(c) Uanzishwe mpango maalum wa kuwafanyia uchunguzi watoto wanaozaliwa ili kubaini kama wanao ugonjwa huo toka awali ili hatua zichukuliwe bila kuchelewa,(d) Serikali na wadau wengine wa Sekta ya Afya waangalie uwezekano wa kuwa na kampeni za kuelimisha umma juu ya ugonjwa huu kama inavyofanyika kwa magonjwa mengine kama cancer,malaria,kipindupindu,(e) Uangaliwe uwezekano wa kuanzisha shule maalum kwa ajili ya watoto wenye magonjwa yasiyotambulika.


Baadhi ya wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye mkutano huo.
Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo.

Jeedygirl katika picha ya pamoja na Monica Joseph

C.E.O wa Life Goes On Blog niliwakilisha 
 

Baadhi ya Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.PICHA NA MICHUZI JR-MMG

No comments:

Post a Comment