Ukosefu wa ajira ni changamoto kubwa duniani kote.
Hili linasikitisha kwa kuwa kazi ni chanzo cha heshima binafsi, amani na
utulivu.Tanzania,
miongoni mwa nchi za dunia ya tatu, imechukua hatua muhimu katika
kuendeleza sekta yake ya ajira, japo bado inakabiliwa na changamoto
kubwa katika hilo. Asilimia kubwa ya watanzania wenye uwezo wa kufanya
kazi, aidha hawana ajira au ajira walizonazo haziendani na uwezo wao.
Kutokana
na ushindani mkubwa katika soko la ajira na ongezeko kubwa la vijana
wanaoingia kwenye soko la ajira (800,000 hadi 1,000,000 kwa mwaka),
sekta rasmi imekosa mafanikio katika kuzalisha fursa za ajira, hasa
mijini. Matokeo yake ni; kiwango cha umasikini kimeongezeka.
Sababu kuu zinazochangia fursa duni za ajira ni pamoja na:
· Kutokuwa
na usawa kati ya supply ya wafanyakazi na mahitaji. Ukweli ni kwamba,
supply ya wafanyakazi ni kubwa kuliko demand ya wafanyakazi katika soko
la ajira. Kila mwaka tunashuhudia ongezeko la vijana wanaomaliza masomo
yao ambao wanaingia mtaani kuongeza idadi ya watafutao kazi.
· Vijana
kukimbilia kutafuta kazi mijini. Asilimia kubwa ya vijana wakimaliza
elimu yao, hufikiria kwenda mijini kutafuta ajira, na wengi wao huwa na
mawazo ya kufanya kazi ‘za ofisini’. Hili linasababisha shinikizo na
ushindani mkubwa wa fursa za ajira. Laiti kama vijana wengi wangeamua
kujikita katika sekta ya kilimo cha kisasa au sekta nyingine tofauti
tofauti kwa kutumia elimu yao, ongezeko la watafutao kazi mjini
lingepungua kwa kiasi kikubwa.
· Elimu
duni. Hili linajumuisha kutokujua kusoma na kuandika na ukosefu wa
mafunzo sahihi yanayomuandaa mtu kuingia katika soko la ajira. Hakuna
mwajiri anayeweza kuajiri mtu asiye na stadi muhimu za kitaaluma
zinazohitajika katika kazi. Inaaminika kuwa, zaidi ya 61% ya wahitimu
wanakuwa hawako tayari kiushindani katika soko la ajira.
Kutokana na mwangaza huo wa hali halisi ya ajira nchini Tanzania mradi wa #RecruitMe umejipanga
kusaidia kila mwenye uwezo wa kufanya kazi, vijana na wazee ili waweze
kupata ajira wanazotaka. Tunafahamu kwamba ukosefu wa kazi ni jambo
linalotatiza wengi na wengi kuhisi kuwa wamenyimwa haki yao kama
binadamu ndani ya jamii wanayoishi.
Kwa hiyo, #RecruitMe kwa
makusudi mazima imeamua kujitolea kuweka jukwaa ambalo kila mtu anaweza
kulitumia anapotafuta ajira sahihi na kupitia jukwaa hilo, mtu anaweza
kugundua fursa mpya zilizopo katika soko la ajira. Zaidi ya hayo,
waajiri wanaweza kunufaika sana kutokana na jukwaa hili, kwa kuwa
linatoa fursa kwao pia kutafuta wafanyakazi wanaowahitaji.
Lengo
kuu la mradi huu si kuwapa watu ajira yeyote tu, la hasha, bali ni
kuwapatia watu ajira zenye hadhi, heshima na kufanya ndoto za mtu kuwa
kweli. #RecruitMe itakupatia
ajira inayokubalika kisheria, yenye mapato yanayoendana na kiwango cha
kazi na ujuzi wako. Tunakuthibitishia ajira itakayojali haki zako kama
mwanadamu na mfanyakazi, ikiwa ni pamoja na kujali maslahi yako.
Ili kupata huduma zetu, tafadhali tembelea tovuti yetu http://goo.gl/zPLquy ambapo
utakuwa na uwezo wa kuona fursa za ajira mbalimbali, pamoja na kujenga
profile yako mwenyewe. Huna haja tena ya kutokwa na jasho kutembea
kutoka ofisi moja hadi nyingine tu na kuishia kunyimwa nafasi. Pumzika,
na tembelea tovuti yetu. Tunaweza kukusaidia kupata kazi uitakayo.
0 comentários :
Post a Comment