Thursday, 1 October 2015

WANACHAMA WA CHAMA CHA MAWAKALA WA FORODHA TANZANIA WAJIUNGA NA PSPF

Wanachama wa Chama cha Mawakala wa Forodha Tanzania wameweza kujiunga na mfuko wa Pensheni wa PSPF ili waweze kufaidika na mafao ya mfuko huo katika sherehe zilizofanyika kwenye ukumbi wa Karimjee


Viongozi wakuu wa TAFFA, wakionyesha kadi za uanachama wa mpango wa uchangiaji wa hiari kwenye Mfuko wa Pensheni wa PSPF (PSS), baada ya kukuunga wakati wa mkutano mkuu wa mwaka wa TAFFA. Kulia ni Meneja Matekelezo wa PSPF, Francis Mselem, Meneja Masoko, Mawasilioano na Uenezi, Costantina Martin (wapili kushoto) na meneja wa mpango wa uchangiaji wa hiari (PSS), Mwanjaa sembe


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Florence Turuka, akihutubia wanachama wa chama cha mawakala wa forodha Tanzania (TAFFA), mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa TAFA kwenye ukumbi wa Karimjee .


Meneja Masoko, Mawasiliano na Uenezi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Costantina Martin, akiwaeleza wanachama wa Chama cha mawakala wa forodha Tanzania TAFA, juu ya hufuma mbalimbali zitolewazo na Mfuko huo, wakati wa mkutano mkuu wa TAFFA jijini Dar es Salaam. PSPF na TAFFA wamefungua ukurasa mpya wa mahusiano ambapo wanachama kadhaa wa TAFA walijiunga na Mfuko huo




Baadhi ya wanachama wa TAFFA wakiwa kwenye mkutano huo


Wanachama wa TAFFA wakijiandikisha na mfuko wa Pensheni wa PSPF


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Florence Turuka, akisikiliza maelezo kuhusu huduma mbalimbali zitolewazo na Mfuko wa Pensheni wa PPF, kutoka kwa afisa wa Mfuko huo, Delphin Richard, mara baada ya kufungua mkutano mkuu wa TAFFA, ambapo PSPF ilitumia fursa hiyo kueleza shughuli zake 



Picha ya pamoja

No comments:

Post a Comment