PSPF YATOA MSAADA WA MAGODORO CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM

MFUKO wa Pensheni wa PSPF, umekipatia Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, UDSM, magodoro 118 ili kusaidia huduma ya malazi kwa wanachuo walioathirika kutokana na bweni lao kuungua moto kwenye hosteli ya chuo hicho Mabibo jijini Dar es Salaam Aprili mwaka huu.
Akikabidhi msaada huo kwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Profesa David A. Mfinanga, Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Abdul Njaidi, amesema, PSPF, iliguswa na ajali hiyo ya moto ambayo iliyotokea  kwenye bweni kitalu namba B na kusababisha mamia ya wanachuo kupoteza mali zao.
“Kwa kutambua kuwa wanachuo ni sehemu ya jamii ya Watanzania, na pia ni wanachama watarajiwa wa Mfuko, tumeona tuchangia sehemu ya vifaa ili wanafunzi waweze kurejean katika hali yao ya kawaida.” Alisema Njaidi.
Pichani ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam, (Anayeshughulikia masuala ya Utawala), Profesa David Mfinanga, (Watatu kushoto), akipeana mikono na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Abdul Njaidi, (watatu kulia), wakati akipokea msaada wa magodoro 118 yaliyotolea wan Mfuko huo kwenye hafla fupi iliyofanyika chuoni hapo. Magodoro hayo ni kwa ajili ya wanafunzi walioathiriwa na moto uliozuka kwenye bweni kitalu B kule hosteli za Mabibo,mnamo Aprili mwaka huu 2015.


Akitoa shukrani zake, kwa niaba ya Chuo, Profesa Mfinanga aliishukuru PSPF, kwa msaada huo ambao kwa hakika umesaidia pakubwa, kwani magodoro hayo yatapelekwa kwa walengwa na hivyo kusaidia kuwapunguzia machungu waliyoyapata kutokana na kuunguliwa vifaa vyao.
Kwa mujibu wa viongozi wa Chuo hicho, jengo hilo lilikuwa ,linakaliwa na wanachuo 788, wakati linawaka moto.

Pichani Profesa mfinanga (wapili kushoto), akitoa shukrani kwa niaba ya chuo mbele ya maafisa wa PSPF,  viongozi wa wanachuo na wafanyakazi wa chuo hicho wakati wa hafla hiyo
 Afisa Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Abdul Njaidi, (kushoto), akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, baada ya kukabidhi msaada huo, Agosti 24, 2015
 Meneja wa malazi kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Paulina Mabuga,  (wapili kulia), akizungumza kwenye hafla hiyo. Wakwanza kushoto ni Rais wa Serikali ya Wanafunzi, Denis Bashulula
 Profesa Mfinanga na Njaidi wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa serikali ya wanafunzi UDSM
Magodoro yaliyo tolewa na mfuko wa PSPF
 
Kwa kweli ni jambo jema lakuigwa na jamii kwani PSPF wameweza kuwa mfano bora.
Life Goes On .......

About life goes on

Blogger | Journalist | Entrepreneur | Fashonista Based in Dar es Salaam, Tanzania.

0 comentários :

Post a Comment