Thursday, 16 July 2015

BINTI WA ISSA MICHUZI AJITOSA KUWANIA UBUNGE VITI MAALUMU TABORA

Zahara Michuzi ni binti wa Issa Michuzi blogger ambaye ni mpiga picha hodari wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Mrisho Kikwete ambaye anamalizia muda wake sasa. Binti wa Michuzi mara baada ya kuhitimu elimu yake ya shahada yake ya uchumi UDOM ameona ni vyema akawatumikua wananchi wa nyumbani kwake mkoani Tabora kwa kutangaza nia ya kugombea ubunge wa viti maalum kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi.

 Zahara akiifurahia form yake ya Ubunge wa viti maalum Tabora.
 Binti huyo wa Michuzi akikabidhiwa form yake leo katika ofisi za UVCCM mkoa-Tabora
Zahara akikabidhiwa form ofisi za UVCCM mkoani Tabora.

Nawasihi watanzania haswa tulioko Tabora tujitokeze kwa wingi na tumpatie kura zetu binti wa Michuzi nimsomi, mpiganaji na mchapakazi. Tumwezeshe na tumpe nafasi atuwakilishe vijana wa Tabora maana maendeleo ni muhimu mwaka huu na kipindi chote cha uongozi wake tumwamini kwa hili.

No comments:

Post a Comment