Thursday, 11 December 2014

TASWE SACCOS IMEKUJA KUFANYA MAGEUZI

Mwenyekiti mtendaji wa IPP Media, Dk Reginald Mengi amezinduwa Tanzania Saccos For Women Entrepreneurs (TASWE -Saccos) jana tarehe 10, Desemba, 2014 katika ukumbi wa St. Peter Oysterbay jijini Dar es salaam, itakayo wezesha watanzania na wanachama kuweka akiba, kukopa na kununua hisa kwa ajili ya kupata mitaji ya kuboresha shughuli zao za kijamii na kiuchumi.
Mwenyekiti wa TASWE Saccos mama Anna Matinde amewakaribisha wananchi wote wajiunge na mfuko huu wa Saccos kuepukana na riba kubwa wanazo zipata kutoka taasisi nyingine ili kuweza kujikwamua kimaisha.
Nanukuu msemo wa mheshimiwa Dk Reginald Mengi... I WILL, I CAN, I MUST I AM NUMBER ONE !!!!






No comments:

Post a Comment