Tuesday, 25 November 2014

WHERE IS HUMUNITY????



Video above shows how house girl miss treat, abuse a small child while are parents are off to job



Siamini binadamu mwenye akili timamu anaweza kufanya unyama kwa mtoto mdogo malaika asiye na hatia unyama wa kiasi hiki.

We insist all working parent to put camera on their absent because we don't know what our kids going through behind.

  

Thanks God she is fine a bit scared of people, but the house girl she still at police station

Polisi wamebadilisha mashtaka ya
mfanyikazi wa nyumbani aliyenaswa kwa kamera akimpiga na kumtendea
unyama mtoto wa mwaka mmoja na nusu, kutoka kwa kosa la kutesa na sasa
anakabiliwa na kosa la jaribio la mauaji.






Video hiyo iliwaudhi watu wengi sana kwenye mitandao ya kijamii ila
babake mtoto huyo alisema walisambaza video hiyo ili kuwatahadharisha
wazazi wenegine.



Mfanyakazi huyo wa nyumbani Jolly Tumuhirwe, alikuwa amezuiliwa katika
gereza la Luzira na mahakama ya Nakawa kwa kosa la kutesa chini ya
kifungo cha 41 kwenye katiba kinachoongelea dhidi ya mateso.



Mwanamke huyo sasa anatarajiwa kufikishwa mahakamani tarehe 8 Disemba.

Hata hivyo, msemaji wa polisi Bwana Fred Enanga, amesema "shtaka dhidi
ya mwanamke huyo lilibadilishwa baada ya kupitiwa mwendesha mkuu wa
mashitaka.



Tumuhirwe alikubali kosa la kumpiga mtoto huyo kwa kurunzi, tuki
olililonaswa kwa kamara ya CCTV. Polisi walimfanyia Tumuhirwe uchunguzi
wa kiakili na kubaini kuwa ana akili timamu.



Afisaa mkuu wa polisi Fred Enaga, amewaonya waajiri kuchunguza mbinu
zinazotumika kuwachagua wasichana wa kazi, kwa sababu matendo kama haya
yanaweza kutokana na matatizo ya kisaikologia.



Waziri wa Jinsia, Kazi na maendeleo ya jamii Bi Mary Karooro Okurut
alipongeza juhudi za wazazi wa mtoto huyo Arnella "kutokana na kitendo
hicho kwa mtoto.



 Ingekuwa mtu mwingine angemuua mischana huyo wa kazi lakini alifuata
sheria. Pia tunapeleka marekebisho katika katiba kuhusu maslai ya watoto
bungeni kuimarisha sheria zinazowajali watoto," alisema waziri huyo.



Polisi wamesema kuwa nia ya shambulio hilo haijatambulika na pia
msichana huyo amefanyia kazi familia hiyo kwa siku 26 pekee. Wazazi
wamesema kuwa mtoto huyo ametolewa hosipitalini na hali yake ya afya
inaimarika.



Kulingana na msemaji wa polisi Fred Enaga, kesi hiyo iliripotiwa na Baba
ya mtoto Erick Kamanzi mnamo tarehe 13 Novemba katika kituo cha polisi
cha Kiwatule baada ya kuona video hio.



Kesi hiyo ilipelekwa kwa kitengo cha polisi cha Kiira. Baada ya
uchunguzi, msichana huyo wa kazi alihukumiwa na shataka la mateso katika
mahakama ya Nakawa na kuzuuliwa katika gereza la Luzira.



Bwana Enaga alisema Bi Tumuhirwe alishtakiwa chini ya kifungo cha tatu
kwenye katika kinacholinda maslahi ya watoto. Kifungo hicho kinajumuisha
mashataka kama ya kutesa inayopeana uwezekano wa kumfunga mtu hadi
miaka 15 gerezani.



Hata hivyo, Bwana Enaga anashauriana na mkurugegenzi wa pande za mashtaka kurebisha hukumu hilo kuwa kifungu cha maisha. 


 





No comments:

Post a Comment