Thursday, 12 December 2013

HAKI ZA WATOTO ZIKO WAPI? MTOTO AZRA ANATESEKA JAMANI

MTOTO ALIYEZALIWA MAHABUSU ATIMIZA MIAKA 2 AKIWA MAHABUSU SABABU WAZAZI WAKE WANATUHUMIWA KUKUTWA NA MADAWA YA KULEVYA HUKO MBEYA.

 Hapa mtoto Azra Vuyo Jack akiwa na umri wa miezi 5. 

Nimesikitishwa mno na hii habari nimeamua kukujuza na wewe hufahamu this is how life goes on hapa hapa Tanzania yetu......

Maskini kichanga hiki hakijapata malezi mazuri amekosa haki zake zote za msingi kwakuwa mama yake na baba yake wana kesi ya kukutwa na madawa ya kulevya nchini Tanzania. Inasemekana mama si raia wa Tanzania ni mtu wa Afrika kusini lakini je ubalozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania unafahamu juu ya mtoto Azra? Naamini haki ya binadamu ni sawa na haki ya watoto haichagui huyu katokea taifa gani au la.. je shirika la haki za binadamu na haki ya watoto inafahamu juu ya hilo? this is life goes on huko mahabusu na kwenye magereza watoto wanazaliwa na kujikuta wanatumikia adhabu ambazo haziwahusu. This is too bad naomba vyombo husika litupie macho juu ya hili suala.

  

Mtoto Azra akiwa na wazazi wake nje ya mahakama wakisubiria mwendelezo wa kesi yao.

Hapa kakiwa kadogo kabisa naamini angekuwa mtanzania nchini Afrika kusini amefikwa na haya basi fasta fasta jitihada zingefanyika na angekombolewa hau mtoto angerudishwa nchini na angepata ungalizi mzuri tu hata wa watu kujitolea. Hii inanifanya niamini wabongo ni wakatili kuliko taifa lolote la afrika. Kwanini wao watuhurumie siye na kila siku watu wetu wanakamatwa afrika ya kusini kwa kesi za madawa ya kulevya kila siku tunasikia vijana wanakamatwa na haichukui muda mrefu tunaona jitihada za serikali yetu kwenda kuwakomboa iwaje siye tufumbie macho juu ya mtoto Azra?

Yapata miaka miwili sasa mtoto Azra anateseka mahabusu jijini mbeya nafahamu atakuwa anaishi maisha hatarishi na pia itakuwa inamuathiri sana kisaikologia inahuzunisha kwakweli.

 

Pichani ni mtoto Azra akiwa anamiaka miwili sasa nje ya mahakama jijini mbeya ambako kesi ya wazazi wake ikiendelea huko akiwa na mwandishi wa MBEYA YETU BLOG.

Mtoto Azra ni mfano wa watoto wengi tu ambao hatujawafahamu bado lakini wanakosa haki zao kwa kuishi magerezani na mahabusu wakati hawana hatia hili hali vituo vya kulea watoto viko vingi sana.

 Jamani Haki Ya Watoto Hawa Hiko Wapi?

No comments:

Post a Comment