Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amefika katika makazi ya Kiaskofu ya Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam, Kurasini, kuwasilisha salamu za rambirambi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kufuatia kifo cha Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo.
Makamu wa Rais akizungumza na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam, Mhashamu Askofu Yude Thaddeus Ruwa’ich (OFM Cap), amesema Rais Samia ameguswa na msiba huo na kuahidi kushirikiana bega kwa bega na Kanisa Katoliki katika msiba huo.
Amesema Serikali inatambua mchango mkubwa aliyoutoa Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo katika kipindi cha miaka 42 ya utumishi wake na nia ya Serikali ni kuona kwamba Kardinali Pengo anazikwa kwa heshima zote.
Kwa upande wake Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam, Mhashamu Askofu Yude Thaddeus Ruwa’ich (OFM Cap), ameishukuru Serikali kwa mchango iliyotoa wakati wa matibabu ya Kardinali Pengo.
Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, alifariki tarehe 19 Februari 2026 katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Jijini Dar es Salaam.

.jpeg)

.jpeg)

0 comentários :
Post a Comment